Mkuu wa Wilaya ya Hanang',Ghaibu Buller Lingo ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara katika Mji mdogo wa Katesh wilayani Hanang' Mkoa wa Manyara.
Amesema kwamba, ni vyema kila mmoja ajenge utamaduni wa kulipa kodi zake kihalali bila kutumia njia za ujanjaujanja ambazo haziwezi kumfikisha mahali popote.
Lingo amesema, endapo wafanyabiashara hao watakuwa waaminifu katika kulipa kodi za biashara zao wanazofanya,zitasaidia kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya,maji na miundombinu ya barabara.
“Kwa hiyo niwasihi ndugu zangu tuwe wazalendo kwa kumuheshimu Mungu kwa sababu Serikali hizi zimnetoka kwa Mungu, kwa kulipa kodi zetu bila kutimiza ujanjaujanja,kwani mnapotimiza ujanja tukiwagundua Serikali kutumia kidogo vyombo vyake mnaanza tena kupiga kelele,na mimi nisingependa kutumia sana vyombo, labda ninyi mkinilazimisha,"amesema Lingo.
Mkuu huyo wa wilaya amekiri pia kwamba, vitambusho vinavyotumiwa na wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga,vitaendelea kuboresha zaidi ili kuondoa changamoto zilizopo kwenye vitambulisho hivyo.
Lingo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Hanang' amefafanua kuwa, mauzo ghafi chini ya shilingi milioni nne yanahitaji kuwa na vitambulisho ingawa vitambulisho hivyo bado wataendelea kuviboresha kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwa na picha,majina huku wengine wakiazimana wanapokuwa wakifanya biashara zao.
“Na Rais wetu mpendwa Dkt.John Pombe Magufuli alisema bado atatoa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo na mtu akiwa na kitambulisho asibughudhiwe,"amesema.
Rose Kamili ambaye ni mfanyabiashara na mkulima wa mazao pamoja na kumpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kuwaunganisha na kuwafanya wafanyabiashara hao waweze kufahamiana,lakini alilalamikia kukosekana kwa soko la zao la vitunguu,na hivyo kumuomba afike Kata ya Basutu kuzungumza na wakulima wa zao hilo. Habari mpya endelea kusoma hapa.
Pia wafanyabiashara hao pamoja na kuridhishwa na utaratibu ulioanzishwa na Mkuu wa wilaya huyo wa kukutana na makundi mbalimbali, lakini pia wamesema huyo ni mkuu wa wilaya wa kwanza tangu wilaya ya Hanang' ilipoanzishwa kukaa nao na kuwashauri waunde umoja wa wafanyabiashara kwa maslahi mapana ya wafanyabiashara na Taifa.