Fatma Karume ambaye alizaliwa 15 Juni 1969 ni mwanasheria wa Kitanzania na wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019.
Alipata wadhifa huo baada ya kushinda katika uchaguzi wa urais wa chama hicho uliofanyika Aprili 2018 na hivyo kumrithi mtangulizi wake Tundu Lissu aliyekiongoza chama hicho kutoka mwaka 2017 hadi 2018.
Fatma ni mtoto mkubwa wa Rais wa Awamu ya Sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume na ndugu zake wengine ni Abeid, Shuwana na Ahmed.
Ni mjukuu wa Rais wa Awamu ya Kwanza wa Zanzbar, Sheikh Abeid Aman Karume.
Kwa upande wa elimu yake ya masuala ya kisheria kwa kiasi kikubwa amesomea nchini Uingereza.Amefanya kazi kwa muda mrefu katika Kampuni ya IMMA Advocates ya jijini Dar es Salaam katika kusimamia masuala ya mashitaka mahakamani kabla ya uamuzi tajwa juu kufanyika.
|