Kazi iendelee; Mgombea Urais Dkt.John Magufuli aandikisha historia ya kipekee Uwanja wa Lake Tanganyika, asema mambo mazuri yanakuja



Sehemu ya wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma leo Septemba 18,2020.


Amesema, katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali yake imepanga kununua meli mbili ambazo zitafanya kazi katika Ziwa Tanganyika ili kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo.

Dkt.Magufuli amesema, meli mmoja itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 400 na abiria 600 huku meli nyingine itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 4,000 hatua ambayo itakuwa ya mafanikio zaidi.
Pia amesema mbali ya kununua meli hizo pia, Serikali yake imepanga kuzifanyia matengenezo meli za MV Liemba na MV Sangara na kiasi cha shilingi Bilioni 16 zitatumika.

"Leo tarehe 18 mwezi wa 9 andikeni kuwa tunayosema yanatoka moyoni, mimi sitoi ahadi hewa, nataka Kigoma mfanye biashara , tunanunua meli mpya mbili , nimechoka kusikia ajali kwenye Ziwa Tanganyika, hivyo tunataka kutengeneza muelekeo mpya wa Kigoma," amesema huku akiongeza kuwa mpango mwingine ni kujenga ofisi kubwa ya bandari ambayo itahudumia bandari zote zilizopo Ziwa Tanganyika yakiwemo majengo mengine muhimu.
Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Kigoma waliofurika katika Uwanja wa Lake Tanganyika katika mikutano ya kampeni za CCM mkoani Kigoma leo Septemba 18,2020.



Sehemu ya wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma leo Septemba 18,2020.


Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimvalisha kofia msanii wa kizazi kipya Linex mara baada ya kutumbuiza katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news