Kupitia mtanange huo uliochezeshwa na refa Hussein Hamisi wa Katavi aliyesaidiwa na Joseph Masija wa Mwanza na Robart Rwemeja wa Mara, bao pekee la Yanga SC limefungwa na kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Serge Mukoko Tonombe 73'.Huenda kampeni zinazoendelea Ukanda wa Magharibi kwa vyama mbalimbali vya siasa vimeichanganya timu ya Kagera Sugar, ni baada ya wageni wao Yanga SC kuwacharaza kwa bao moja kwa buyu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Ushindi huo wa Yanga SC katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukaba, Kagera unaifanya kuwa na alama saba hivyo kuifanya klabu hiyo inayofundishwa na kocha Mserbia, Zlatko Krmpotic kukwea kileleni.
Ushindi huo wa Yanga SC katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukaba, Kagera unaifanya kuwa na alama saba hivyo kuifanya klabu hiyo inayofundishwa na kocha Mserbia, Zlatko Krmpotic kukwea kileleni.
Ni baada ya mechi tatu huku ikishinda mbili na sare moja katika mechi zake mbili za awali nyumbani katika jiji la Dar es Salaam.
Kabla ya mechi Mtibwa Sugar walipasha kwanza kujiweka sawa. |
Kiungo huyo kupitia bao hilo alisababisha kubadilika kwa mfumo wa mchezo wa kujihami wa Kagera Sugar tangu mwanzoni mwa mchezo na wao kuanza kwenda kushambulia moja kwa moja hali ambayo imeongeza burudani zaidi, ingawa jitihada za kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime hazikuzaa matunda.
LINE UP! KAGERA SUGAR FC
CHALAMANDA
MWAITA
LUHENDE
KYARUZI
SONSO
UFUDU
KAGAWA
SESEME
MWATEREMA
MO IBRA
MAYANGA
SUBS
TINOCCO
ISIHAKA
MWALYANZI
KAPAMA
MBARAKA
SADAT
MWIJAGE
Aidha, mchezo uliotangulia leo mchana, Tanzania Prisons ilipata ushindi wa kwanza baada ya kuwachapa Namungo FC moja kwa buyu, bao pekee la Gasper Mwaipasi 47' katika Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
Prisons wanafikisha alama nne baada ya mechi tatu, kufuatia kufungwa na kutoa sare mechi mbili za awali ugenini, wakati Namungo FC, wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho msimu huu wanabaki na pointi zao tatu kufuatia kufungwa mechi nyingine moja nyumbani na kushinda moja.
Hata hivyo, baada ya mechi hizo, Simba SC watamenyana na Biashara United ya Musoma mkoani Mara na Coastal Union wataikaribisha Dodoma Jiji Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wakati Mbeya City watamenyana na Azam.
Raundi ya tatu itakamilishwa Jumatatu kwa michezo mingine miwili, Ruvu Shooting na Gwambina Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Mwadui FC watawakaribisha KMC Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.Yanga wamevuka kidogo, Simba itakuwaje leo tuziachie 90' uwanjani.
Tags
Michezo