Maalim Seif amnadi Tundu Lissu Zanzibar, abainisha atakavyoboresha kilimo cha mananasi, matikiti kuanzishwa kilimo cha maua

Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemnadi mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrsia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu katika mkutano wake wa kampeni na kueleza kuwa ana imani atakuwa Rais wa Tanzania, anaripoti Talib Ussi (Diramakini) Zanzibar.

Maalim Seif aliyaeleza hayo katika Uwanja wa Mpira wa Mwanakombo katika Jimbo la Mohonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja katika mfululuzo wa kampeni zake visiwani humo.
Amesema hana wasiwasi kuwa, Lissu atakuwa Rais na amesema akiingia madarakani mgombea huyo wa CHADEMA na yeye akiwa Rais wa Zanzibar siku ya pili tu baada ya kuapishwa atamtaka amkabidhi Mashekhe wa Zanzibar ambao wamewekwa ndani Tanzania Bara.

“Imani yangu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na mimi nitakuwa wa Zanzibar itakuwa raihisi Mashekhe wetu kuwarejesha,"ameeleza Maalim Seif.

“Lakini ikitokea bahati mbaya akirudi huyo Magufuli na mimi nikiwa Rais nitamtumia ndege, lazima awatowe watu wangu,”amesema.

Pia Maalim Seif katika masuala ya kilimo amesema, endapo atapata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar ataboresha sekta ya kilimo kwa kujenga viwanda vidogo vidogo kwa ajili kuhifadhia mazao.

Amesema, kama sekta ya kilimo itatazamwa kwa jicho la kimaendeleo inaweza kuwa chanzo kingine cha uchumi na kuwapatia ajira wananchi waliowengi.

“Zanzibar tumejaaliwa kuwa na matunda mazuri kama vile matikiti na mananasi, lakini serikali iliyopo inaangalia tu, nikiingia madarakani lazima tuwe na mpango maalumu wa kuyasimamia ili wananchi wetu wapate pato bora,”ameeleza Maalim seif.

Amesema, matikiti na manansi yanafikia kuharibika kwa kukosa soko na kudai kuwa mara akiingia Ikulu atahakikisha wakulima wa kilimo hicho watatafutiwa masoko.

Sambamba na hilo Maalim Seif ameeleza kuwa, atawashawishi wakulima wa Zanzibar kujingiza katika kilimo cha maua kwa kutumia Greenhouse.

Amesema, kilmo hicho ni maarufu ulimwenguni kote na kina uwezo wa kufanya Wazanzibar kusafiri nje ya nchi kwa ajili kilimo hicho tu.

Amesema, nchi nyingi zinaongeza pato la taifa lao kwa kutumia kilimo hicho cha maua ambacho kama watu watawezeshwa ni kilimo rahisi sana

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news