Maalim Seif: Nitafuta wingi wa kodi, Kitambulisho cha Mkaazi, walimu wa Madrasa watalipwa mishahara

Mgombea Urais Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema wingi wa kodi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekuwa ni kikwanzo kwa wafanyabiashara kukuwa kiuchumi, anaripoti Twalib Ussi (Diramakini).

Maalim Seif ameyaeleza hayo katika Viwanja vya Kiungoni Jimbo la Pandani Wilaya Wete Pemba wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho waliojitokeza kwa wingi katika kuendeleza kampeni zake kisiwani Pemba.

Amesema kutoka na mzigo huo wa kodi kwa wafanyabiashara ni kwamba wafanyabiashara wengi wamefunga biashara zao kutokana na mzigo mzito wanaotwisha na Serikali iliyopo madarakani.

Amesema kuwa, mara kwa mara Serikali wanasema uchumi unakuwa, lakini wananchi wa kawaida wanazidi kuumia huku hali ya maisha ikizidi kuwa ngumu.

"Wenzetu waliopo kwenye madaraka wanajali kipato cha Serikali tu na kuwanyonya wananchi mpaka wanafunga biashara zao,"amesema.

Amesema kuwa, ni lazima katika serikali yake kuondoa kodi zote ambazo hazina msingi kwa wafanyabiashara na serikali.

Mapema Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo alifanya ziara ya kutembelea maduka ya wafanyabiashara wa Kijiji cha Kiungoni Wilaya Wete na kupokea malalamiko mengi yanayohusiana na kodi.

“Licha ya kuiona biashara imeshuka kwa mfanyabiashara, lakini ZRB wanataka kiwango kile kile walichojiwekea bila kujali hali halisi ilivyo, hili katika serikali yangu lazima liondoke,”ameeleza Maalim Seif.

Katika hatua nyingine Maalim Seif amezungumzia suala la elimu ya dini na kudai kuwa waliopo kwenye madaraka wameitupa elimu hiyo.

Amesema, walimu wa Madrasa wamekuwa watu maskini licha ya kazi kubwa wanayoifanya katika kuwapitia elimu yenye manufaa yake ya Dunia na Akhera.

“Madrasa zetu lazima tuzingalie kwa jicho la kiungwana na kuwalipa walimu wa Madrasa kama vile wanavyolipwa waimu wa shule.

“Tutahakikisha nao wanakaa kwenye viti na meza sio kugaragara kwenye mchanga utamaduni huo lazima tuuondoshe katika Serikali mpya nitakayoiongoza,”amesema.

Pia Maalim Seif ameeleza kuwa, katika Serikali hatabaguwa dini nyingine na atakaa na viongozi wa dini nyingine ukiachana na Uislam ili kujua matakwa yao katika dini zao waweza kyuatekeleza.

Amesema katika utawala wake anataka kila mwananchi aheshimu dini ya mwenzake kama ilivyokuwa zamani kwa Wakirsto.

“Ikiingia Ramadhani Wakristo walikuwa wanakula ndani ya majumba yao na ulikuwa hauwaoni wakila jiani ovyo kutokana kuheshimu dini ya wenzao,”amefafanuwa Maalim Seif.

Pia Maalim Seif amesema akiingia madarakai ataondoa Kitambulisho cha Mkaazi na kuweka kitambulisho cha raia wa Zanzibar kwa ajili ya utabuzi wa rai wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news