Mwanasheria wangu, Ndugu Omar Said Shaaban ambaye ndiye aliyeniwakilisha kwenye kusikiliza na kujibu pingamizi zilizowekwa dhidi yangu akinikabidhi rasmi barua ya uteuzi wangu wa kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Mapambano yanaendelea!
Baada ya uamuzi huu ambao ulitangazwa saa 12 jioni unamfanya Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mtu wa 17 na katika nafasi ya urais ikiwemo kufunga pazia.
Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa ametangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) baada ya kukamilisha zoezi la kupitia na kuchambua taarifa za pande zilizohusika na pingamizi aliyokuwa amewekewa awali.
Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo, Omar Said Shaaban amesema kwamba, uamuzi wa ZEC ulizingatia kuwa kile kilichoitwa 'taarifa za uongo' kwenye fomu za uteuzi za mteja wake hazikuwa na mashiko kwa kuwa hata kama zingekuwa za kweli, basi hazikulenga kumnufaisha mgombea huyo.