Maalim Seif:Wazanzibari msifanye makosa, dhamira yangu ni kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi barani Afrika, Zanzibar Airlines inakuja, mashirika ya meli ndege yatafutiwa kodi zinazowatatiza

Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi barani Afrika, anaripoti Talib Ussi (Diramakini) Zanzibar.

Maalim Seif ameyaeleza hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Alabama karibu na maeneo ya Michenzani Wilaya Mjini Unguja jijini Zanzibar.

Maalim Seif amesema, anakusudi kuifanya Zanzibar kuwa na bandari ambayo wafanyabishara wataweza kuingiza bidhaa zao bila ushuru na wakati wa kutoa watatozwa ushuru mdogo sana.

Amesema, akilifanya hilo wafanyabishara wa nchi za Afrika Mashariki na Kati wataweza kuingia Zanzibar na kujipatia bidhaa zoote wanazozitaka kwani ushuru utakuwa mdogo sana.

“Kama jamaa zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda na wengineo wamekuwa wakienda Dubai kufuata bidhaa ninaimani wananchi kama mtanichagua watakuja Zanzibar kufuata bidhaa hizo,”ameeleza Maalim Seif.

Amesema kuwa, anashangazwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushindwa kujenga bandari katika eneo la mpiga duru kwa muda wote huo tangu walipoeleza.

“Niliwaambia hawa hawana uwezo, kwani wakinyoshewa kidole na viongozi wao wa Tanganyika hawafanyi kitu, lakini nikiingia madarakani tu lazima tujenge bandari ya Kimataifa katika eneo hili,” alieleza.

Amesema kuwa, kwa sasa Bandari ya Malindi haina tena uwezo wa kuhimili meli za makontena na kudai kuwa ikikaa meli moja tuu nyingine zikaa kwenye nanga.

“Tunakusudia kuijenga bandari ambayo itaweza kubeba zaidi ya meli sita za makontena kwa wakati mmoja,”amesema Maalim Seif.

Ameeleza kuwa, Serikali ACT Wazalendo inakusudia kujenga Bandari ambayo mashirika ya meli za Kimataifa yatapata hamu ya kushusha mizigo yao Zanzibar.

“Kwanza tunakusudia kuondoa vikwanzo vyote ambavyo vinayafukuza mashirika ya meli au ndege kuja katika nchi yetu, tutashusha kodi ambayo itawafanya waridhike kuja kwetu,”amesema.
Sambamba na hilo Maalim Seif ameweka wazi kuwa katika miaka yake mitano atahakikisha Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ambalo litatembea duniani kote.

Asema kuwa, yapo makampuni mengi yako tayari kuingia ubia na serikali ili kuazisha shirika hilo.

“Tutakuwa na shirika letu la ndenge ambalo tutaliita Zanzibar Airline, hili litasaidi sana kuongeza watalii nchi mwetu,”amesema Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo.

Akilitilia mkazo hilo ameelezwa kuwa, shirika hilo pia itaisaidia Zanzibar kujitangaza ulimwenguni na watu wengi kupata hamu ya kuingia visiwani humo.

Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa aliuwambia umma kuwa anakusudia kupanga upya uwanja wa ndege wa Zanzibar ili uwe na uwezo wa kubeba ndege nyingi kwa wakati.

“Nipeni kura zenu halafu muone nitakavyoibadilisha Zanzibar kuwa kama nchi ya Singapore kwa maendeleo na muenekano wake kwa ujumla,”ameeleza Maalim Seif.

Amesema,vijana ni nafasi yao kupata ajira kwa kila mmoja na zenye heshima kupitia mikakati hiyo kabambe.

Maalim anaendelea na kampeni zake katika kisiwa cha Unguja baada ya kukamilisha awamu ya kwanza katika kisiwa cha Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news