Maharusi wakatisha ndoa baada ya kubainika ni ndugu wa damu Kenya

ANN Magwi na Jonathan Munini kutoka nchini Kenya wamelazimika kukatisha zoezi la kufunga ndoa baada ya James Sidai kujitokeza kanisani na kusema yeye ndiye baba yao mzazi.

Maajabu haya! Baba huyo mzazi aliingia kanisani akiwa na dada yake na kusema ndoa hiyo isifungwe kwa kuwa maharusi ni ndugu wa damu.

Amesema,"mama yenu ninyi ni mmoja aliniacha akaondoka na mtoto akiwa na mwaka mmoja, mwingine aliona uchumi wangu umeyumba akaondoka akiwa na mimba ya miezi minne na akaolewa na mwalimu.

"Nikaamua kumuoa mwingine na tuna watoto watatu, nimeona tangazo la harusi yenu WhatsApp zile picha nikasema hawa ni wanangu nikachunguza kwa watu mlioishi nao wakasema ni kweli,"amesema James Sindai.

Hali hiyo licha ya kuzua taharuki, bwana harusi na mtarajiwa wake walitengana hapo na mmoja kuondoka kwa hasira.Endelea

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news