JESHI la Polisi mkoani Tabora limethibitisha taarifa za kukutwa watu wanane ambao wamekufa katika Hifadhi ya Isawima iliyoko wilayani Kaliua mkoani humo.
Watu hao wamekutwa wameungua vibaya, maelezo hayo yakiwa ni kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, ACP Barnabas Mwakalukwa.
Amesema, tukio hilo lilitokea Septemba 6, mwaka huu majira ya saa 11.30 jioni katika hifadhi hiyo iliyopo wilayani Kaliua.
Kamanda Mwakalukwa amesema, maafisa wake walipata taarifa hizo kutoka kwa msamaria mwema aliyekuwa anatafuta mifugo yake katika eneo hilo ambapo aliona watu wamekufa ndipo akafikisha taarifa hizo kwenye Serikali ya kijiji cha Wacha Waseme na kituo cha polisi mjini humo.Habari mpya soma hapa.
Amesema kuwa, baada ya kupata taarifa hizo walielekea eneo la tukio na kuanza uchunguzi ambapo walibaini kuwa kati ya watu hao waliouawa watatu wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 40.
Alisema, wengine ni watoto watano wenye umri wa kati ya miaka miwili hadi 10 ambao miili yao ilikuwa imeharibiwa vibaya na moto huo.
Kamanda amesema kuwa, waliouawa inasadikiwa kuwa ni watu wa familia moja na sababu ya kuchomwa moto haijajulikana, hivyo uchunguzi unaendelea ili kujua chanzo huku akisisitiza kuwa hakuna aliye juu ya sheria, hivyo watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo watawajibika
Maiti nane zaokotwa hifadhini, polisi waonya
Tags
Habari