Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar Rais Shein amnadi Dkt.Hussein Mwinyi Kaskazini Unguja

Umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwa katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar,Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi uliofanyika katika Uwanja wa Mpira Nungwi leo Septemba 20,2020.(Ikulu).
Wasanii wa Kikundi cha Sakakasi kutoka Mkwajuni Unguja wakionesha umahiri wa mchezo wa sakakasi wakati wa hafla ya Mkutano wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Uwanja wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Septemba 20,2020.(Ikulu).
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia na kuwapungia mkono wana CCM wakati akiwasili katika Uwanja wa Mpira Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja katika hafla ya Mkutano wa kampeni ya CCM uliofanyika
leo Septemba 20,2020.(Ikulu).
Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika Uwanja wa
Nungwi kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar leo Septemba 20,2020.(Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dkt.Hussein Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika viwanja vya mpira Nungwi kuhudhuria Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar leo Septemba 20,2020.(Ikulu).
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Mabodi wakiwa katika jukwaa kuu wakati wa hafla ya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa mpira Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Septemba 20,2020.(IKulu).
Viongozi wakiwa katika Jukwaa Kuu. (Ikulu).

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Bongio Fleva IT akitoa burudani kwa wanachama wa CCM katika mkutano wa Kampeni ya Mgiombea Urais wa Zanzibar iliofanyika katika Uwanja wa Mpira Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Septemba 20,2020.(Ikulu).
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Dkt.Hussein Ali Hassan Mwinyi  akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  katika mkutano wake wa kampeni  na kuomba kura kwa wanachini uliofanyika katika Uwanja wa Mpira Nungwi.(Ikulu).

Picha mbalimbali zikionesha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) wakiwa katika Mkutano wa kampeni kuwanadi wagombea wa nafasi ya Urais,Ubunge,Uwakilishi na Udiwani katika viwanja vya Mpira Nungwi Wilaya ya Kaskazini A.Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Septemba 20,2020. (Ikulu).

Katika mkutano huo,wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi wote wametakiwa kuwapigia kura za ndio wagombea nafasi za uongozi katika chama hicho ili kiendelee kuyatunza Mapinduzi ya Januari 12, 1964, kuutunza Muungano,amani,umoja,utulivu na mshikamano na kuendelea kuleta maendeleo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa wito huo leo huko katika mkutano wa Kampeni za (CCM) zilizofanyika Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambao mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho pamoja na mamia ya wanaCCM na wananchi.

Katika maelezo yake, Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar alisema kuwa kwa upande wa nafasi ya Urais Dk. Hussein Mwinyi ndie pekee anaeweza kuyatekeleza hayo yote na hakuna kiongozi mwengine anaeweza kutekeleza hayo miongoni mwa viongozi wanaogombea nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM alieleza kuwa Dk. Hussein Mwinyi ana sifa zote za kuwatumikia wananchi kwani kazi ya urais ni majukumu mazito ambayo yeye anayaweza na kutokana na sifa alizonazo ndio maana CCM ikampa nafasi hiyo ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar na kuwataka wananchi kumpigia kura za kishindo katika uchaguzi ujao.

Wembe uwe ule ule au ikiwezekana kuliko ule .Urais si asali kama kila mmoja arambe,alisisitiza Dk. Shein.

Aidha, Rais Dk. Shein alisema kuwa Dk. Hussein Mwinyi ana sifa maalum na anaweza kuiongoza Zanzibar kwani kwa siafa alizokuwa nazo hakuna hata mmoja anaeleza kumfikia miongoni mwa viongozi wanaogombea nafasi hiyo.

Alisema kuwa Ilani na Sera za CCM ni nyenzo muhimu za kukuza na kuimarisha uchumi na maendeleo ya Tanzania, hivyo ni jambo la muhimu kuendelea kuiunga mkono CCM ili izidi kuzitekeleza na kuwaletea maendeleo wananchi wote kwani Wazanzibari wote wanapenda maendeleo.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwaombea kura viongozi wa CCM wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea wake Mwenza Mama Samia Suluhu Hassan, mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, Wabunge, Wawakilishi pamoja na Madiwani.

Wakati huo huo, Makamo Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar aliwanadi wagombea wote wa CCM pamoja na kuwakabidhi Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ili wakainadi huku wagombea hao wakiahidi kwenda kuifanyia kazi ipasavyo.

Nae Mgombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM Hussein Ali Hassan Mwinyi aliwaeleza wananchi wa Nungwi kuwa changamoto ya maji ataipatia ufumbuzi wa haraka mara tu itakapoingia madarakani Serikali ya Awamu ya Nane.

Alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Saba imeweza kufikisha maji kwa asilimia 72 katika maeneo ya vijijini na kubakisha asilimia 28 ambapo tatizo hilo la maji litapatiwa ufumbuzi mapema sana pamoja na vitega uchumi vyote vya maeneo hayo.

Alieleza kuwa kutokana na utalii kutonufaisha wazawa inavyotakiwa kwani bado kuna changamoto ya ajira ambapo wajasiriamali wadogo wadogo shughli zao hazijawa na tija kwa kutokuwa na soko la uhakika la kufanya shuguli zao vizuri hivyo, wawekezaji wote watawekewa utaratibu maalum wa kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa pale walipoekeza.

Aliongeza kuwa katika suala zima la ujuzi, Serikali itaweka kipaumbele ili vijana waweze kuajirika kwa kuwafundisha elimu za ufundi ili waweze kuajirika na kujiajiri wenyewe ili kuondoa tatizo hilo la watu kutonufaika.

Kwa uande wa wajasiariamali wadogo wadogo kutokana na tatizo la mitaji na ujuzi kutokana na shuguli wanazozifanya alisema kuwa kazi itafanywa kwa kutafuta masoko na kupeleka bidhaa zao katika mahoteli yaliopo katika maeneo hayo.

Alisema kwua kwa upande wa wavuvi alisema kuwa mkazo utawekwa katika uchumi wa buluuu ambapo uvuvi wa bahari kuu utaimairishwa na wavuvi wadogo wadogo wa Zanzibar watapewa nafasi ya kufanya shughuli hizo kwa kuwezeshwa kupewa vyombo vya kisasa, masoko, viwanda vya kusindika samaki ili soko liwe zuri na bei iwe nzuri.

Dk. Mwinyi aliwahakikishia wananchi wa Nungwi na Mkoa wote wa Kaskazini Unguja kuwa iwapo wataichagua CCM changamoto zote hizo zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Alisema kuwa kwa upande wa changamoto ya barabara za ndani ufumbuzi utapatikana kwa haraka kwani tayari barabara kubwa zimeshafanyiwa kazi kwani mpaka hivi sasa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kilomita 129 zimeshajengwa zikiwemo barabara kuu ambapo tatizo bado lipo kwa upande wa barabara za ndani.

Alisema kuwa barabara za ndani zinazopeleka watalii na wananchi wanazozitumia kwa shughuli zao kila siku zitashughulikwia kwa kutiwa lami kwani kazi kubwa imeshafanywa na Awamu ya Saba, hivyo Awamu ijayo itakamilisha.

Kwa upande wa migogoro ya ardhi alisema kuwa atahakikisha kuwa analipatia ufumbuzi kwani hasa katika maeneo ya uwekezaji kumekuwa na tayizo kwa baadhi ya wawekezaji kushirikiana na baadhi ya viongozi kuwapora wananchi ardhi zao bila ya kuwapatia fidia stahiki hasa katika vijini vya Nungwi na Matemwe.

Alisema kuwa suala la ardhi katika nchi yoyote ni rasilimali inayotakiwa kunufaisha wananchi wake lakini kwa wawekezaji wanahitajika lakini haina maana kwamba Yule anaetoa ardhi yake kwa muwawekaji asipate fidia stahili, atahakikisha kwa wale wote waliodhulumiwa kwa namna moja ama nyengine basi wanapata haki yao stahiki.

Aidha, alisema kuwa kwa upande wa suala zima la udhalilishaji Serikali ijayo pamoja na kushirikiana na wananchi wote, itahakikisha inaweka sheria kali sana dhidi ya matatizo hayo, na watendaji wanayashughulikia kwa haraka bila urasimu na kuhakikisha suala hilo linamalizika katika jamii.

Kwa upande wa wajasirialamui wakiwemo waanika dagaa, wauuza bidha za kitalii, mama lishe, wachuuzi,bodaboda, watembeza utalii na wengineo bado shughuli zao hazijawa na tija ya kutosha, atahakikisha wanapewa elimu, mafunzo ili wazifanye kazi zao vizuri zaidi sambamba na kupata mitaji kupitia Benki, Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi pamoja na kujiunga katika vikundi ili iwe rahisi kusaidika.

Alieleza kuwa Serikali ijayo ya Awamu ya Nane itahakikisha inawatafutia masoko na wawekezaji wote wanaelekezwa kuwapa masoko, kuhakikisha kwamba wawekezaji wote wanawapa masoko wao kabla hawajanunua bidhaa kwengine.

Alisema kuwa viongozi wa CCM wataendelea kuzungumzia Ilani na Sera za CCM na hawatowazungumzia watu na wataendelea kuwaambia wananchi nini watawafanyia na iwapo wataendelea kuwaamini na kukiamini chama hicho kitaendela kufanya kazi kwa bidii kwani wagombea wake wamegombea nafasi hizo ili wapate kuwatumikia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news