MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewaomba Watanzania kuwachagua wagombea wanaotokea chama hicho ili wamalizie kazi nzuri waliyoianza.
Aidha amepongeza Rais Mstaafu,Dkt. Jakaya Kikwete kwa kuwa karibu na wananchi wa Chalinze na Bagamoyo, hali inayochangia kuonekana Bagamoyo kuwa ngome imara ya chama hicho.
Samia ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Polisi Chalinze, ambapo mbali ya Rais pia alimnadi mgombea Ubunge Ridhiwani Kikwete, Madiwani wa Kata na Viti Maalumu huku akisema chama hicho kimefanya mambo mengi.
"Ndugu zangu Wanachalinze na Bagamoyo sote ni mashahidi kwa kujionea Serikali yetu chini ya Rais wetu John Magufuli inavyofanyakazi zake, miradi mingi imetekelezwa, mingine iko katika hatua za kumalizika, niwaombe mumchague tena mgombea wetu John Magufuli, wabunge na Madiwani ili tumalizie kazi iliyobaki,"amesema Samia.
Kwa upande wake Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete aliwataka wa-Tanzania kuendelea dumisha umoja, upendo na mshikamano, utaowapatia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu unaotataji utaofanyika Oktoba 28,mwaka huu.
Kikwete amesema kuwa, kura za maoni ndani ya chama zimekwisha, hivi sasa chama hicho kinatafuta ushindi kwa wagombea wake wote kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani, huku akieleza kuwa Serikali imefanya mambo makubwa.
“Kura za maoni zimemalizika, sasa jukumu letu ni moja tu la kumpigania mgombea wetu wa Urais, Mwenza wake, wabunge na madiwani ili tupate ushindi mnono, kwani umoja wetu ndio ushindi wa chama chetu kiweze kuendeleea kushika dola," amesema Kikwete.
Ameongeza kuwa k,nongwa za kura za maoni ni kujimaliza kisiasa, na kwamba ni sawa na vita vya panzi ambavyo ndio furaha ya kunguru, huku akiwataka wana-CCM na wa-Tanzania kwa ujumla waungane kuwachagu viongozi hao, huku akitaka kura zaidi ya asilimia 84 za Magufuli za mwaka 2015 sasa iwe zaidi ya 90.
Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Chalinze anayetetea nafasi hiyo,Ridhiwani Kikwete, alimuomba Makamu wa Rais kuangalia namna ya kuwaongezea ardhi wananchi waishio vijiji vinavyozunguka msitu wa Zigua kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
“Mheshimiwa Mama Samia, kwanza naishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli, tumeona vijiji vingi vinavyozungukwa na hifadhi vimepatiwa ardhi, nami nikuombe ukamfikishie ombi letu, katika hifadhi ya Zigua kwani kuna moja ya Kijiji Zahanati imechukuliwa na hifadhi hiyo,"amesema Ridhiwani.

Wakati huo huo Makamu wa Rais, Samia Suluhu amewahutubia maelfu ya wananchi Kibaha Vijijini kama inavyoonekana katika picha chini.Katika picha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wa Jimbo la Kibaha Vijijini Wilayani Kibaha mkoani Pwani wakimsikiliza Makamu wa Rais na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akiwahutubia leo katika kampeni zinazoendelea kuelekea Oktoba 28,2020.
Tags
Siasa