KUFUATIA kusambaa taarifa za kutekwa kwa kiongozi wa maandamano nchini Belarus, Maria Kolesnikova na watu wasiojulikana ikiwemo kukamatwa kwa wanaharakati wengi wa kisiasa nchini humo, imeendelea kuzua maswali mengi, huku onyo likitolewa.
Maria Kolesnikova Msemaji wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Peter Stano amesema, umoja huo una taarifa kuhusu madai ya kutekwa kwa mwanaharakati huyo pamoja na wanaharakati wengine wa kisiasa.
Stano amesema,wanachokishuhudia ni mwendelezo wa ukandamizaji unaofanywa na mamlaka dhidi ya raia na kuelezea wasiwasi kuhusu kuendelea kwa hatua hizo zinazochukuliwa kwa mirengo ya kisiasa jambo ambalo amesema halikubaliki.
Taarifa za Maria Kolesnikova kutekwa na watu wasiojulikana katikati ya mji mkuu wa Belarus, Minsk na kumpakizwa kwenye gari zimenea zaidi ndani na nje ya Taifa hilo.
Kwa mujibu wa shirika huru la habari la Tut.By la Belarus kutoka nchini humo limeripoti kuwa, baada ya Maria kutekwa na kupakiwa kwenyeb gari, watu hao wasiojulikana waliondokana naye.
Tags
Kimataifa