JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, limefanikiwa kumkamata, Ahmada Daud Mwita (26) mkazi wa Sogea kwa kosa la wizi wa Vespa, ambayo ni mali ya Bakar Omar Saleh (43) mkazi wa Sogea.
Kamanda Awadh amesema, baada ya tukio la wizi kufanyika, Vespa hiyo ilifichwa kwenye nyumba inayomilikiwa na Khalifa Mussa huko Mpendae Unguja.
Amesema, inasadikika kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuiba Vespa hiyo aliamua kuificha mbali na makazi yake, ili kuzuia watu kumuona, na muhusika kuigunduwa mali yake ilipo.
Kamanda alieleza kuwa, ilipofika Septemba 4, mwaka huu, majira ya saa 03:30 asubuhi waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na vespa hiyo maeneo ya Mpendae kwa Kificho.
Aidha,emesema upelelezi wa kesi hiyo unaendelea, na ukikamlika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.