KWA mujibu wa Afisa kutoka TAMISEMI ambaye ni miongoni mwa wawezeshaji wa mafunzo,Sweetbert Kashaija,mfumo wa MadeniMIS utatumika kuratibu madeni na madai ya watumishi wa Serikali yasiyo ya mshahara kwa nchi nzima, lakini kwa kuanzia utaanza na madeni ya walimu.
Wakati hayo yakijiri Busega, www.diramakini.co.tz inakupeleka moja kwa moja mkoani Ruvuma ili kuona namna ambavyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyoazimia kuratibu madai na madeni ya watumishi yote yasiyo ya mishahara kwa njia ya kieletroniki.
Mwezeshaji wa mafunzo ya mfumo huo kutoka TAMISEMI,Nestory Mgimwa akitoa mafunzo kwa wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea amesema kundi la kwanza kunufaika na mfumo huo ni walimu na wanatarajia kupata matokeo chanya.
Amesema, Serikali imeanza kuratibu madeni hayo kwa lengo la kuyatambua na kuyaingiza kwenye mfumo wa MadeniMIS ili kupata takwimu sahihi za madeni halali ya watumishi na kukabiliana na udanganyifu wa madeni hewa ambayo huwa ni kikwazo kwa taifa.
Amezitaja faida za mfumo huo kuwa ni kuongeza uwazi, uwajibikaji, ari ya kufanya kazi na kuondoa usumbufu na gharama kwa watumishi wakati wanafuatilia stahiki za madeni yao.
“Wanufaika wa kwanza kwenye mfumo huu ni walimu ambao ni asilimia 52 kati ya watumishi wote wa halmashauri nchini,”amesema.
Amesema,watumishi katika mfumo huu wanatakiwa kutoa taarifa za ukweli na sahihi katika kudai madai yao kwa kuleta viambatanisho stahiki na kwamba ni kosa la kisheria kugushi nyaraka kwa lengo la kujipatia malipo.
Ubunifu huu wa kuratibu madai na madeni ya walimu umeanza Agosti 3,mwaka huu na unatarajia kukamilika Agosti 18,2020 katika mikoa yote nchini Tanzania.
Amesema,mfumo huu utapunguza malalamiko ya madai na madeni kwa watumishi wa Serikali ikiwa ni jitihada za Serikali kuhakikisha inaboresha huduma.
Baadhi ya watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakipatiwa mafunzo ya mfumo wa madeni ya watumishi Serikalini unaojulikana kama MADENI MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM (MadeniMIS) ambao una lengo la kuhakiki na kuthibitisha madeni ya watumishi.
Afisa huyo amesema,mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili wilayani Busega katika ukumbi wa shule ya Msingi Nyashimo (TRC). Mafunzo haya yameanza kutolewa jana tarehe 8 Septemba, 2020.

Ruvuma
Mwezeshaji wa mafunzo ya mfumo huo kutoka TAMISEMI,Nestory Mgimwa akitoa mafunzo kwa wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea amesema kundi la kwanza kunufaika na mfumo huo ni walimu na wanatarajia kupata matokeo chanya.
Amesema, Serikali imeanza kuratibu madeni hayo kwa lengo la kuyatambua na kuyaingiza kwenye mfumo wa MadeniMIS ili kupata takwimu sahihi za madeni halali ya watumishi na kukabiliana na udanganyifu wa madeni hewa ambayo huwa ni kikwazo kwa taifa.
Amezitaja faida za mfumo huo kuwa ni kuongeza uwazi, uwajibikaji, ari ya kufanya kazi na kuondoa usumbufu na gharama kwa watumishi wakati wanafuatilia stahiki za madeni yao.
“Wanufaika wa kwanza kwenye mfumo huu ni walimu ambao ni asilimia 52 kati ya watumishi wote wa halmashauri nchini,”amesema.
Amesema,watumishi katika mfumo huu wanatakiwa kutoa taarifa za ukweli na sahihi katika kudai madai yao kwa kuleta viambatanisho stahiki na kwamba ni kosa la kisheria kugushi nyaraka kwa lengo la kujipatia malipo.
Ubunifu huu wa kuratibu madai na madeni ya walimu umeanza Agosti 3,mwaka huu na unatarajia kukamilika Agosti 18,2020 katika mikoa yote nchini Tanzania.
Tags
Uchumi
Usajili wa madeni si hoja hoja no kulipa hayo madeni kwa wakati.
ReplyDelete