MGODI WA GGML WAMWAGA MILIONI 800 KUJENGA KIJIJI CHA MAONESHO GEITA

Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu wa Geita (GGML) umetoa shilingi milioni 800 kwa ajili ya kuanzisha Kijiji Maalum cha maonyesho kinachoendelea kujengwa katika Mtaa na Kata ya Bombambili Mjini Geita,anaripoti Robert Kalokola (Diramakini) Geita.
Jengo la Utawala katika Kituo cha Mamlaka ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA) katika Kijiji cha maonyesho ambalo limejengwa kwa fedha kutoka GGML.( Robert Kalokola/Diramakini).

Akizungumza katika Maonyesho yanayoendelea katika eneo hilo Afisa Mawasiliano wa GGML Theophil Pima, amesema kuwa mgodi huo umetoa fedha hizo ikiwa ni moja ya mkakati wake wa kusaidia jamii inayozunguka mgodi huo.

Ameongeza kuwa, katika kuandaa maonyesho hayo pia GGML imechangia milioni 200 ili kufanikisha kazi hiyo ambayo inaratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Theophil Pima ameongeza kuwa,mgodi huo umekuwa unatenga na kutoa jumla ya Bilioni 9.2 kila mwaka kwa miaka mitatu sasa kwa Halmashauri ya mji wa Geita na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Afisa Mawasiliano kutoka Mgodi wa GGML,Theophil Pima akizungumza na vyombo vya habari katika jengo la Utawala la Mamlaka ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA) ambalo liko ndani ya Kijiji hicho cha maonyesho Mjini Geita. (Robert Kalokola/Diramakini).

Akizungumza na Wakuu wa Wilaya Chato,Nyang'hwale,Mbogwe na Geita waliotembelea Kijiji hicho na Mabanda ya Maonyesho Septemba 19 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi,Robert Gabriel amesema kijiji hicho kitakuwa na ukubwa wa ekari 100.

Aliongeza kuwa kutakuwa na huduma kama mabenki,wanyamapori,burudani,kumbi za mikutano pamoja eneo la maonyesho yenyewe.

Aliongeza kuwa kijiji hicho kimeanza kutumika rasmi mwezi huu kwa ajili ya Maonyesho ya teknolojia ya madini ambayo yameanza Septemba 17,mwaka huu na yanatarajiwa kuhitimishwa Septemba 27,mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema kuwa eneo hilo litakuwa na majengo mbalimbali na maeneo ya vivutio vingine.

Jengo la EPZA la utawala katika Kijiji hicho linajengwa chini ya ufadhili wa fedha za uwajibikaji kwa jamii(CSR) kutoka mgodi wa kuchimba Dhahabu wa Geita (GGML) kwa usimamizi wa Halmashauri ya mji wa Geita.

Maonyesho ya teknolojia ya madini na Uwekezaji katika Mkoa wa Geita yalikuwa yanakuwa yanafanyika katika kiwanja cha CCM Kalangalala kwa awamu mbili.

Maonyesho hayo yamedhamiwa na wadau mbalimbali wakiongozwa na na wadhamini wakubwa amabao ni GGML na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Meneja wa Tawi la Geita Benki ya NBC, Hilda Bwimba akizungumza na vyombo vya habari katika jengo la Utawala la Mamlaka ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA) katika Kijiji cha maonyesho Mjini Geita. (Robert Kalokola/Diramakini).

Meneja wa NBC tawi la Geita,Hilda Bwimba amesema pamoja na kuchangia maonyesho hayo Benki hiyo imeendesha mafunzo kwa wajasiliamali na Wachimbaji wadogo.

Ameongeza kuwa,wamejipanga kuhakikisha wanamfuata kila mjasiliamali mahali alipo kwa ajili ya kumjengea uwezo.

Maonyesho hayo yamelenga kuwakuatanisha pamoja wajasiriamali wa aina mbalimbali hususani sekta ya madini ili kubadilishana uzoefu,teknolojia lakini pia masomo ya bidhaa zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news