Mgombea CHADEMA, Leonce Marto ataja vipaumbele 14 kuelekea Oktoba 28

Mgombea Udiwani katika Kata ya Nduli kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leonce Marto amevitaja vipaumbele vyake 14 vya kimaendeleo katika kata hiyo ikiwemo tatizo la migogoro ya ardhi, anaripoti Fredy Mgunda kutoka Iringa.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa kampeni kuwania udiwani wa Kata ya Nduli amesema kuwa, wananchi wa kata hiyo wanakabiliwa na tatizo la mtandao wa maji kwenye mitaa, hivyo akipewa ridhaa na wananchi wa kata hiyo atahakikisha anatatua kero hiyo.

Amesema kuwa, ili shughuli za kimaendeleo ziendelee kwa wananchi bila mkwamo wowote ule ni lazima tatizo la maji litatuliwe kwa wakati ili kupisha shughuli nyingine za kimaendeleo ziendelee.

Mgombea udiwani katika Kata ya Nduli kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leonce Marto akiomba kura kutoka kwa wananchi wa Kata ya Nduli walipojitokeza kwenye ufunguzi wa kampeni za Jimbo la Iringa Mjini. (Diramakini).

Marto amesema kuwa, kata hiyo inakabiliwa na migogoro mingi ya ardhi kutokana na uwepo wa viongozi ambao hawasimamii vizuri mipango bora ya matumizi ya ardhi, hivyo kuanzisha migogoro mingi.

"Nikipewa ridhaa ya kuwa diwani kata hii ya Nduli nitahakikisha natoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi bora ya ardhi,uuzaji na ununuaji wa ardhi kuepuka dhuluma ambayo inasababisha migogoro hiyo,"amesema Marto.Amesema kuwa, atahakikisha anatatua na kuboresha sekta ya elimu kuanzia miundombinu ya majengo na kutoa bonanzi kwa walimu na wanafunzi shule za msingi ili kuboresha ufaulu na utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi.

Aidha Marto amesema kuwa, kata hiyo bado inategemea kilimo kwa asilimia kubwa, hivyo ni lazima kuhakikisha wakulima wanalima kilimo cha kisasa na chenye faida kwa wakulima hao ilikiwa sambamba na kuboresha miundombinu ya barabara kwa lengo la kurahisisha usafiri.

Marto amesema kuwa, suala la michezo,mikopo,huduma ya afya,masoko,wazee,yatima,wananchi wasio wenye uwezo yaani masikini,kuboresha mawasiliano ya simu kwa wananchi wa kata hiyo, hivyo vyote vitaboreshwa ili kuchochea maendeleo ya wananchi wa Kata ya Nduli.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news