Mgombea Ubunge kupitia CCM Priscus Tarimo ataja vipaumbele vinavyogusa namna ya kuwavusha vijana kutoka umaskini hadi utele Moshi Mjini

Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana wa Moshi litatafutiwa ufumbuzi wa kina kwa kupatiwa ajira katika kiwanda cha Ngozi cha Karanga mkoani Kilimanjaro,anaripoti Pius Ntiga,Moshi.

Kiwanda hicho cha Ngozi Karanga kilichopo Mjini Moshi ambacho kimeanza kufanya kazi za awali kitakuwa na uwezo wa kuzalisha ajira 3,000 ambapo kati ya hizo ajira 2,000 zitawanufaisha vijana wa Moshi Mjini.

Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Soweto Mjini Moshi ambao pia umehudhuriwa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, Heri James.
Katika ufafanuzi wa ahadi hiyo amesema, uwepo wa kiwanda hicho cha ngozi Karanga atahakikisha akifika Bungeni endapo atashinda Ubunge atalisimamia suala la upatikanaji wa ajira hizo 2,000 kwa vijana wa Moshi.

Pia amesema atahakikisha Mji wa Moshi unakuwa ni wa Viwanda kwa kushirikiana na serikali ili kuvifufua viwanda vilivyokufa.

Pia atahakikisha vijana wanaoongoza watalii wanapata mikataba ya kudumu sanjari na kuwawezesha kimtaji wajasiriamali na akina mama lishe na watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM, Heri James ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM, amewataka wananchi wa Moshi wasifanye makosa Oktoba 28,mwaka huu na badala yake wawachague wagombea wanaotokana na CCM.

Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatatajiwa kufanyika Jumatano ya tarehe 28 Oktoba,mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news