Mgombea Ubunge kupitia NCCR-Mageuzi Kennedy Chaya ataja vipaumbele 15 vya kihistoria Jimbo la Malinyi

"Ndugu wananchi wa Wilaya ya Malinyi kwa majina naitwa Chaya Kennedy Mgombea Ubunge Jimbo la Malinyi kupitia tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, nipo hapa leo kuwaambia ndugu zangu wa Malinyi kwamba ifikapo Oktoba 28,mwaka huu siku ya kupiga kura, kura zote za ndiyo nipigie mimi Chaya Kennedy wa NCCR-Mageuzi na kuwa mbunge jimbo hili la Malinyi kwa miaka 2020-2025, anaripoti Mwandishi Diramakini.
"Naiomba nafasi hii ya Ubunge nikiamini kutokana na uzoefu wangu katika masuala ya kisiasa huku nikisukuwa na dhamira na nia ya dhati kutoka moyoni mwangu ya kuwatumikia wana Malinyi katika nafasi hii ya ubunge, lengo likiwa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo 

"Ndugu wananchi wa Malinyi kitaluma mimi ni mwandishi wa habari kwa miaka mingi niko kwenye tasnia hii ya habari nikijikita zaidi kiuchambuzi, nikiandika habari za afya, elimu, mazingira na siasa, huku habari zingine nikiandika pia, hivyo ndugu wananchi uzoefu wangu katika siasa hauna shaka hata kidogo, mkinichagua hakika mtakuwa mmempata mwakilishi mzalendo mwenye kiu ya maendeleo katika jimbo letu la Malinyi.

"Aidha, kupitia taaluma yangu hii nimekuwa nikifanya kazi kwa ajili ya Malinyi nakumbuka katika hekaheka za kupata Wilaya ya Malinyi kulikuwa na sarakasi nyingi, nilitumia kalamu yangu kuandika umuhimu wa kuwepo Halmashauri ya Malinyi huku Dkt.Haji Mponda Mbunge aliyemaliza muda wake akitumia 'reference' ya makala zangu bungeni kushawishi Serikali iridhie kuipitishwa Malinyi kuwa halmashauri na hatimaye mwaka 2015 tukapata halmashauri, Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akaipitisha Malinyi na kuwa wilaya mpya.

"Nataka niwambiae leo hiii unaweza kumuuliza maneno haya DktMponda, Mbunge aliyemaliza muda wake, anaweza kukataa, sitashangaa kwa sababu tunatofautiana itikadi, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli na yeye atakuwa anajua ukweli kwamba nilifanya kazi hiyo kwa ajili ya Malinyi.

"Sambamba na hilo nimekuwa nikiripoti matukio mbalimbali ya furaha na huzuni kama migogoro ya wafugaji na wakulima, mafuriko na nyinginezo.

"Ndugu wananchi wa Malinyi, mimi ni mzawa nimesoma, nimeishi ninayejivunia kuifahamu vizuri Jimbo la Malinyi, lakini kabla sijaomba nafasi hii nilijiuliza sana kwamba Malinyi inahitaji Mbunge wa namna gani, jibu nilipata ilihitaji Mbunge mzalendo,mnyenyekevu,mwadilifu na mwenye maono ,anayejua mahitaji ya Malinyi kwa sasa,ilipo na inakoelekea, neema ilioje ndugu wananchi mimi ndiye aina ya Mbunge ambaye Malinyi inamuhitaji kwa sasa,usifanye makosa Oktobar 28 chagua Chaya Kennedy.


"Ndugu wananchi nagombea nafasi hii nikisukumwa na kauli mbiu ya chama chetu kuwa 'Utu ndiyo itakadi yetu pamoja tutashinda', kiongozi mwenye utu atafanya kwa ajili ya leo,kesho na siku zote kubwa zaidi atajali shida za wananchi anawaongoza na kwa pamoja Malinyi tutashinda yote sisi kama NCCR-Mageuzi tunayaishi maneno haya kila kitu kizuri kitakachopatikana Malinyi tugawane wote Wanamalinyi,ubinafsi kwetu mwiko Malinyi si ya mtu bali Malinyi ni yetu sote.

"Ndugu wananchi wa Malinyi yapo mambo nimejipanga kuyafanyia kazi mara tu mkinipa ridhaa ya kuwa Mbunge wenu kama vipaumbele vyangu ambavyo ni;

UJENZI WA MIUNDO MBINU

Ndugu wananchi natambua jimbo au Wilaya ya Malinyi ina changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara hasa wakati wa masika, mvua zikinyesha barabara za ndani kutoka kata moja hadi nyingine barabara huwa hazipitiki,ubovu wa madaraja na nyingine na hasa hii barabara kubwa ambayo imekuwa kero kwa sisi wakazi wa Malinyi ni hii ya Malinyi hadi Ifakara naifahamu hiyo kero ndugu zangu nikiwa Mbunge nitaipambania hiyo barabara ndani ya Bunge na nje ya Bunge.

"Nawaahidi ndugu zangu watu wa Malinyi miaka mitano ya uongozi wangu bungeni barabara hiyo itakuwa katika kiwango cha lami, kadhalika pia na barabara ya Lupilo Malinyi, Kilosa Mpepo hadi Londo Kitanda, Namtubo Songea(Barabara ya Songea). Barabara hiyo tangu niko shule ya msingi naisikia, nayo nitahangaika nayo nikiishauri Serikali nayo iwe katika kiwango cha lami;

KILIMO

Ndugu wananchi kilimo ndiyo uti wa mgogo wa taifa letu hata sisi watu wa Malinyi, kilimo ndiyo tegemeo letu katika kuendesha maisha yetu, acha niwaambie mkinichagua na kuwa Mbunge wenu nitahakikisha ninyi wapiga kura wangu mnalima kilimo cha kisasa na chenye tija.

"Ndugu wananchi kwa sasa Malinyi zao mama ambalo ndiyo zao la chakula na biashara ni mpunga tunategemea sana kilimo cha zao hilo, mazao mengine kama mahindi na ufuta tunalima kwa mazoea, ndugu zangu tunahitaji sana kuwaza kulima mazao mengine ya kibiashara, neema tulinayo Malinyi tuna ardhi yenye rutuba ambayo unaweza kupanda zao lolote likaota bila msaada wa mbolea kama mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ukiwemo Iringa ,Mbeya Njombe na Ruvuma.

"Tutakapolima mazao ya biashara tutafanya mji wetu wa Malinyi kuwa mji wa kibiashara, hapa tafsiri yake pato la mtu mmoja mmoja litakuwa juu, huo ndiyo wakati tutakaoimba wimbo wa maendeleo kwa kila mmoja, ndicho ninachoamini mimi ndani ya miaka mitano hii mkinipa ridhaa ya kuwa mbunge wenu Malinyi itachanya mbuga kimaendeleo.

"Ndugu wananchi mazao ambayo nitahamasisha kama mazao biashara kwa ushirikiano na baraza la madiwani ukiacha mpunga ni mahindi, ufuta, mtama mbaazi, kunde choroko, mazao haya siku hizi Malinyi hayalimwi sana kwa sababu wananchi wa malinyi wamekosa msukumo na kiongozi wa kuwaongoza katika ulimaji wa mazao hayo.

"Lakini pia wamekuwa wakuongozwa na hadithi za abunuasi kuwa mazao haya hayana mnunuzi nawaambia mazao haya yana wanunuzi wengi, kwani baadhi ya mazao hayo yanatumika katika kutegenezea vitafunio vya chai, sasa mtasemaje yatakosa wananuzi, mimi ndiyo nitawaleteaa wanunuzi wa mazao yenu kazi yenu ninyi ni kunichagua tuu Oktoba 28.

"Kuhusu mahindi soko la la mahindi kubwa lipo jijini Dar es Salaam mbapo mahindi yanaliwa sana ya kuchomwa na hata ugali kwa kiwango kikubwa tukizalisha kwa wingi mahindi Malinyi wafanyabiashara watakuja kununua mahindi kwa wakulima wetu kama wanavyofanya kwa mpunga kadhalika na mazao mengine Malinyi, tuamke tumchague kiongozi mwenye mpango kazi.

Katika mazingira mapato ya halmashauri yataongezeka na hata sisi wananchi, ndugu zangu uwepo wa mwingiliano wa kibiashara wa mazao ya kimkakati niliyoyataja itaisadia sana Malinyi kupata barabara nzuri tena za kiwango cha lami zinazopitika nyakati zote.

"Ndugu wananchi Malinyi ni wilaya tajiri kwa bahati mbaya sana kwa muda mrefu haijapata mwakilishi wa wananchi mzalendo, mimi nakwenda kuwa mbunge mzalendo ambaye nakwenda kufanya kazi za kibunge kwa ajili ya Malinyi.

Aidha. natumbua kuwa Malinyi kuna michikichi mingi (mawese ), mafuta ya mawese ndiyo mafuta ya kula Malinyi yanaliwa kwa wingi na wakazi wa Malinyi nikiwa mbunge tutaanzisha kiwanda cha kisasa cha kuchakacha mawese au michikichi kusudi mafuta hayo wananchi wayauze hata nje ya Malinyi;

UVUVI

Ndugu wananchi wa malinyi tuna mito mingi ambayo huzaliisha samaki wengi katika mazingira kama haya nafahamu sana shughuli za uvuvi zinafanyika na wavuvi wapo kazi yangu kama Mbunge ni kuwasemea na kuwashauri namna bora ya kufanya kazi ya uvuvi,kwa mfano kuwa na vikundi vya wavuvi ambayo vinaweza kukopesheka katika taasisi za kifedha, lengo langu nataka kuona mvuvi wa Malinyi anakuwa na thamani sawa na mvuvi wa Mwanza, Kigoma na kwingineko.

Kuhakikisha zana bora za uvuvi zinapatikana kwa wingi Malinyi ili kuweza kurahisisha shughuli za uvuvi kwa wavuvi wetu, lakini kuipa thamani samaki yetu ya Malinyi shauku yangu ndani ya miaka mitano nataka kuona samaki wetu ya Malinyi wawe wanaliwa mikoa yote hasa Dar e Salaam na mikoa mingine.

Zaidi nataka kuona katika majiji kama Dar es Salaam, Arusha,Mwanza,Tanga, Mbeya watu wawe wanakunywa supu ya samaki za Malinyi kama kitoga,pelege, kambale, njege na nyingine kama inavyofanyika kwa samaki za Mwanza na Kigoma, Sato na Sangara inawezakana sana ndugu zangu watu wa Malinyi.

"Tunayo maeneo mengi ya uvuvi hivyo samaki ni wengi mahitaji yakiwa makubwa tutafikiria pia hata namna ya kuanza ufugaji wa samaki Malinyi ,kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo, uuzaji wa samaki nje ya Malinyi utasaidia mapato kwa wavuvi wetu Malinyi sambamba na pato la Halmashauri ya Malinyi kuongezeka.

Ndugu wananchi kwa mazingira haya yanatusadia sisi watu wa Malinyi kushawishi Serikali kutuletea barababara bora tena za kiwango cha lami, kutokana na rasilimali tulizonazo.

UFUGAJI

Ndugu wananchi Malinyi pia kuna wafugaji, mfugaji anaweza kuwa mtu yoyote Malinyi, lakini zaidi kwa Malinyi wafugaji zaidi ni jamii ya Wasukuma ingawa sasa Malinyi hata makabila kama Wandamba,Wabena na Wapogoro wanafuga pia mifugo inazungumzwa ni ng'ombe,mbuzi, kondoo na mingine.

Kazi yangu nikiwa mbunge wenu nitahakisha wafugaji wanapata haki yao kama wafugaji ili waweze kufuga katika ubora unaotakiwa ili mifugo yao ikiingia sokoni iwe na thamani katika mauzo yaani auzwe kwa bei nzuri itakayomnufaisha mfugaji mwisho wa siku mfugaji maisha yake yawe bora akijivunia kazi yake hiyo ya kufuga.

Lakini nitahakikisha kunakuwepo madawa ya mifugo hapa kwa ushirikishwaji na maofisa wa mifigo ngazi ya wilaya na kata katika kutoa elimu ya mifigo juu ya magonjwa ya mifugo kama ng'ombe, mbuzi kondoo na hata kuku madawa hayo yawepo ya kutosha Malinyi, lakini kuwepo jampo josho la kuogeshea mifugo.

Suala la josho nitalipigania kusudi hata kila tarafa au kata kuwepo na majosho jambo hilo linawezena kama kutakuwepo na viongozi wapenda maendeleo kama mimi, kadhalika natamani kuona maloli ya ng'ombe yakitoka Malinyi kuelekea soko la Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Rasilimali na maendeleo yatakayopatikana Malinyi ndugu wananchi ndiyo yataleta ushawishi kwa serikali kutuletaea barabara ambazo kila siku tunazitamani, lakini ndugu zangu lazima vifanyike vitu vionekane kwa macho ndipo barabara zitakuwepo ili kusudi bidhaa zetu zipite katika barabara nzuri.

ELIMU

Ndugu wananchi wa Malinyi pamoja na Serikali inasema elimu bure kutoka shule za msingi hadi sekondari, lakini zipo changamoto nyingi hususani hapa kwetu Malinyi ikiwemo uhaba wa walimu, walimu wakiwa wachache huduma ya kufundisha watoto wetu inakuwa dhaifu, maana yake pia hata ufaulu unakuwa dhaifu, uhaba wa madarasa, lakini pia vifaaa kufundishia.

Ndugu zangu elimu ni msingi wa maendeleo, huwezi kufanya chochote kama hujapata elimu nawaahidi katika suala hili elimu nikiwa Mbunge nitaishauri Serikali namna bora ya kutengeza mazingira bora ya elimu Malinyi, ujenzi wa shule kila kata hilo nalo nitalisimamamia kwa nguvu zangu zote. Tunahitaji kuwa na elimu bora Malinyi ili vijana wetu waweze kufanya vizuri katika elimu za juu.

"Lakini pia uanzishaji elimu kazi Malinyi hasa kwa wale wanafunzi wanaomaliza darasa la saba, lakini hawajabahatika kufaulu kuendelea na masomo ya sekondari sambamba na wale wanaofeli kidato cha nne.

"Hawa lazima tuwatafutie madarasa ya elimu kazi kufeli mitihani siyo kufeli maisha, lazima tuwe na shule ambayo vijana hao wakitoka moja kwa moja wataenda kufanya kazi binafsi au za kuajiriwa nasisitiza lazima Malinyi kuwepo na vyuo mfano udereva , ushonaji , seremala , ujenzi , hii itawafanya vijana wetu kuwa na kazi ya kufanya

AFYA NA USTAWI WA JAMII

Ndugu wananchi kwa Mujibu wa Wizara ya Afya ya Tanzania kwamba watoto 1-5 matibabu bure sambamba na wezee pamoja na hilo katika sera afya malinyi tumekuwa changamoto ya Watumishi katika zahanati na vituo vya afya viko vituo vya afya katika jimbo letu au wilaya yetu watumishi wachache sana ukulinganisha na idadi ya wagonjwa wanaowapokea kwa siku kwaajiri ya matibabu ,ukosefu wa madawa ya kutosha.

Ndugu wananchi afya ni kila kitu ukiwa na afya mbovu hakuna maendeleo katika mambo ambayo nitapigana kwa nguvu zangu zote nikiwa bungeni Dodoma ni pamoja na suara la afya.

Hospitali ya wilaya ya Malinyi lazima iwe ya hadhi ya kiwilaya ili matibabu ya magonjwa yote kuanziaa matibabu hadi vipimo lakini pia kuwa na matibabu ya kibingwa kwa watu angalau hao madaktari bingwa wawe wanakuja walau mara 2 kwa mwezi itatutusadia sana watu wa malinyi ninawaahidi ndugu wananchi nitayafanyia kazi hayo kwa ajiri yenu

Magonjwa kama Moyo figo ini ni lazma kuwa na mkakati katika hospitali ya wilaya kuhakikisha tunakuwa na klinic ya kibingwa kwa magonjwa hayo ili kusadia wananchi kutambua magonjwa hayo katika hatua za awali na kutibiwa

Malengo yangu kama mbunge mkinichagua nitahakisha kila mwananchi wa malinyi anakuwa na bima ya afya itakayomwezesha kupata matibabu yote hata akiwa nje ya malinyi kwa kutumia kadi ya bima yapo makampuni mengi ambayo mimi kama mbunge wenu nitaingia nayo makubaliano hata NHIF tunaweza kuwa na makubaliano nayo.

UANZISHAJI WA BENKI YA WANANCHI MALINYI
 

Ndugu wananchi wa Malinyi yako mambo mazuri nimepanga kufanya kwa dhati kabisa ya moyo wangu hizi benki ni muhimu sana kuanzishwa kwenye halmashauri kama yetu, benki hizi zimefanyika kuwa msaada kwa wananchi kupitia kazi zao

Benki hizo zipo kwenye Halmashauru kama za Mwanga mkoani Kilimanjaro Mbinga Songea imani yangu wapo wasomi wabobezi katika fedha hata Malinyi tunao wengi wazuri nikiwa mbunge nitawatafuta popote walipo kwa sababu nawajua watatusadia namna bora ya uendeshaji.

Uanzishaji benki hii ndugu wananchi itawasadia sana wananchi wa Malinyi husususani wakulima wadogo wavuvi na wafugaji kuweza kukopesheka kwa masharti nafuu maana saa nyingine kupitia hizi benki za kibiashara mkulima mdogo ni ngumu kukopesheka.

Sasa sisi kupitia benki hii itakuwa rahisi kwa wakulima wa heka moja au mbili kukopeshaka na kulima hadi hekta tano, benki hiyo wanahisa wake ni wakazi na wananchi wote wa Malinyi.

Ndugu wananchi zao kubwa la benki yoyote ni mkopo, lakini pia akaunti hata sisi benki yetu hiyo lazima msingi wetu utakuwa mikopo na akaunti, wananchi wa Malinyi wote watakuwa na akaunti kama amana halafu watakopesheka.

Wananchi watakopeshwa kwa mipango na mikakati itakayopangwa kwa mfano mkulima atakopeshwa wakati wa kilimo na kwa vyoyote malejesho yatakuwa wakati wa mavuno mkulima atatakiwa kulipa mkopo sambamba na riba ndogo na mdhamani wake atakuwa mwenyekiti wake wa kitongoji,kijiji au mtaa.

Kitu ambacho nakifahamu kwa wananchi wa Malinyi hasa wakulima wadogo wameshindwa kufanikiwa kutokana na uwezo wa fedha sasa kupitiaa banki hiyo wakulima wadogo watakopesheka na watalima kilimo cha mashamba mengi mtu ambaye alikuwa analima hekali moja basi alime hadi tano hii ina faida mbili kwanza inaondoa matatizo ya njaa pili linaongeza pato kwa mkulima huyo la zaidi pato la halimashauri liongezeka pia.

Wala asitokee mtu aniambie kuwa jambo hili la kuwa na benki ya wananchi Malinyi haiwezekani kwa sababu,yoyote ile yeye ndiyo atakuwa hawezi lakini sisi kwa umoja wetu tutaweza ngoja nikuambie mtaji namba moja wa uanzishaji wa benki hiyo ni mwananchi wa Malinyi mfano idadi ya watu wazima Wilaya ya Malinyi ni zaidi ya watu 100,000 sasa uandaliwe mpango kupitia madiwani kwa kila kata mwananchi huyo atoe laki moja nusu hapo mtaji hautapatikana? jibu litapatikana.

Lakini jijijini Dar es Salaam siku moja niliwahi kuzungumza na Mkurugenzi wa taasisi moja inayojihusisha na utoaji elimu namna ya uanzishaji wa benki hizo za wananchi, nakumbuka nilimwelewa sana, ndugu zangu wana Malinyi wakati ukifika na mkinichagua haya yote yanawezekana.

UANZISHAJI WA HIFADHI YA MALINYI

Ndugu wananchi wa Malinyi natambua katika wilaya yetu na jimbo letu la Malinyi kuna mbuga kubwa ndani yake kuna wanyama wa kila namna mbuga hiyo ambayo kwa sasa serikali wanaitambua kama pori tengefu, hoja yangu hapa nikiwa mbunge nitaishauri serikali kuona umuhimu wa kuanzisha hifadhi ya Malinyi kwenye hilo pori tengefu ambalo limepita kila kata iliyopo wilayani Malinyi.

"Nafahamu hapa kutakuwa na mjadala mpana kwa kuwashirikisha wadau na wananchi wenyewe kuangalia mipaka kati ya makazi ya watu na hifadhini mwisho wa siku ninaamini kwa kuangalia maslahi mapana na faida iliyopo kwenye hifadhi tunaweza kupata hifadhi siku moja Malinyi.

Umuhimu wa kuwa na hifadhi ndugu wananchi ni nikuleta fedha za kigeni, mapato ya ndani yanaongezeka lakini pia upatikanaji wa ajira. Ndugu zangu mimi naamini haya ninayozungumza yanawezekana kama tukiwa wamoja na kutanguliza malinyi kwanza.

Ndugu wananchi tukiwa na hifadhi malinyi unakuwa mji wa kitalii fedhaa zinakuwa nyingi kutajengwa Mahoteli maendeleo yataonekana ndugu zangu shughuli za kitalii zina fedha nyingi malinyi tutakuwa tunapokea wageni mara kwa mara sasa katika mazingira kama haya kwa nini barabara za lami kama ya Malinyi-Iifakara ambayo ni kero kubwa kwetu na ile ya Lupilo, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo Londo Kitanda hadi Namtumbo (barabara ya Songea).

UWEZESHAJI WA MAKUNDI MBALIMBALI AKINA MAMA VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

Ndugu wananchi nafahamu halmashauri kupitia mapato yake yake ya ndani hutenga asilimia kumi kwa makundi ya kina mama asilimia nne vijana asilimia nne walemavu asilimia mbili, lakini uliza hizi fedha za 4,4,2 kwa miaka mitano hii vikundi vingapi vya akina mama,vijana na watu wenye ulemeavu wamenufaika na fedha hizi.

Ndugu zangu mimi nimezunguka katika jimbo hili kuna vijana, akina mama na walemavu hawajui kwa habari ya fedha hizi kama hawajui nani awaambie na kama hawajui fedha zao zimeenda wapi kuna watu watakuwa na majibu muwaulize, lakini pia muwaulize kwa miaka 5 fedha ngapi zimetumika

Kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia sasa kama ww kiongozi huelezi fursa za fedha za 4,4 2 kwa wananchi wako ww utakuwa kiongozi usiyefaa na viongozi kama hawa ndugu wananchi mpaswa kuwakataa kuwachagua.

Ndugu wananchi mkinichagua na kuwa mbunge nitahakikisha fedha hizo zinafika kwa walengwa kwa wakati ili waweze kunufaika nazo tutaanzisha vikundi vya vijana vingi kila kata kina mama na wezetu wenye ulemavu wataanzisha miradi midogomidogo ya kijasiriamali mimi kama mbunge kazi yangu ni kuwasapoti.

MAJI SAFI NA SALAMA

Maji ni uhai Malinyi kuna changamoto maji safi mabomba mengi za zamani maarufu midundiko iliharibika, hivyo nafahamu wananchi wa wanatembea umbali mrefu kutafuta maji kama mbunge naawahidi suara maji nitalifanyia kazi kwa nguvu zangu zote kuhakisha tanapata ufumbuzi changamoto ya maji

Aidha kupitiaa fedha ya mfuko wa jimbo kwa kushirikiana na madiwani wa halmashauri tutahakikisha tunachimba visima ili wananchi wetu Malinyi wapate maji ndugu zangu mimi kama kiongozi natangulia mbele nalibeba suara la maji mpaka bungeni na kuiomba serikali utusadie kutatua changamoto ya maji , Tunapokuwa na maji safi tuwaepusha wananchi wetu na magonjwa tumbo yanayoambatana na kunywa maji machafu.

VITA DHIDI YA RUSHWA NA UKANDAMIZWAJI

Ndugu wananchi wa Malinyi mimi ni kiongozi ambaye nakataa na kuichukia rushwa sasa ogopa sana kiongozi anayekupa pesa ili mchague agopeni sana hao anakununua baadaye anakutelekeza halafu baada ya miaka mitano anakuja tena anakupa rushwa, nisikilize kataaa viongozi wa namna hiyo kataaa kuuza utu wako kwa fedha

Ndugu wananchi na viongozi wa namna hiyo wakiwa bungeni huwa wanawaza mamilioni ya fedha walizohonga katika kampeni sasa hapo atawaza saa ngapi kuomba maji au umeme jimboni saa nyingine fedha alizotumia kuhonga zinakuwa sio zake kakopeshwa tena kwa riba kataeni viongozi hao, mimi naomba mnichague mimi kijana wenu mzalendo nilete maendeleo katika jimbo hilo.

ULINZI , USALAMA NA HAKI

Ndugu wananchi ulinzi usalama na haki ni vitu ambayo mwana Malinyi anatakiwa kuwa navyo, Malinyi panatakiwa kuwe sehemu salama kwa kila mtu hata kwa wageni, kama Mbunge nitahakikisha hakuna uonevu au kunyima haki bila sababu kuna watu wananyanyaswa na kuonewa bila sababu vitendo hivyo havikubaliki.

Hakuna mtu yoyote yule aliye juu ya sheria ila nawaomba ndugu zangu kila mmoja wetu atii sheria bila sheria na kuheshemu mamlaka zilizopo na wala si kuogopa. Usalama kwa mwana Malinyi pamoja na mali yake ni jambo la muhimu na la kuzingatiwa.

KUTATUA MIGOGORO

Ndugu wananchi nafahamu Malinyi kuna migogoro mingi kama migogoro ya ardhi mipaka na mashamba, migogoro baina ya wafugaji na wakulima katika migogoro hiyo tunatakiwa kufahamu chanzo cha migogoro ni nini ndipo tutafute suluhisho, ndugu wananchi naifahamu Malinyi vizuri kwa hiyo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya tutaweza kutatua migogoro hiyo kwa wakati.

Ndugu wana Malinyi wenzangu wakati mwingine migogoro mingine inatakiwa busara tu kutumika ili itatuliwe kwa mfano migogoro uliyopo pale Kata ya Igawa kati ya Kijiji cha Kiwale na Igawa, Kanisa Katoliki na kijiji cha Igawa pale busura tu inatakiwa kutumika sisi NCCR-Mageuzi tunataka maridhiano, watu wakae pamoja watafute maridhiano. mimi nikiwa Mbunge wenu nitakuwa mstari wa mbele katika kutafuta maridhiono Malinyi ni yetu tuache migogoro isiyo na tija.

UANZISHAJI WA RADIO MALINYI

Ndugu wanannchi mimi nikiwa kama mwanahabari, mkinichagua na kuwa Mbunge nitaanzisha kituo cha radio Malinyi kwa lengo la kutangaza vivutio vilivyopo Malinyi sambamba na kutoa matangazo mbalimbali juu ya elimu, afya, mazingira, siasa na maendeleo pamoja na michezo na burudani.

KUINUA VIPAJI VYA WANAMICHEZO, SANAA NA WASANII

Ndugu wananchi nikiwa kama sehemu ya jamii ya Malinyi nitakuwa jukumu la kuinua vipaji vya wanamichezo, sanaa na wasanii, nikianza na soka mpira wa miguu ambao ndio unapendwa zaidi duniani na hata hapa malinyi

Ndugu wananchi Malinyi kuna vipaji vingi vya mchezo wa mpira wa miguu kwa bahati mbaya sana vipaji hivyo haviendelezwi na matokeo yake vinakufa, ndugu zangu michezo ni biashara na ajira hasa huu mchezo wa mpira wa miguu, nakusudia kuanzisha shule ya michezo na vituo vya michezo hapa Malinyi ili kusudi vijana wetu waweze kuendeleza vipaji vyao.

Nataka niwaaminishe kuwa katika miaka mitano hii mkinichagua na kuwa mbunge nitahakikisha vijana wetu wenye vipaji Malinyi wataenda kucheza mpira timu za ligi kuu kama siyo Simba na Yanga basi timu zingine kama Mtibwa, nk, mniamini inawezekana sana mimi nipo jikoni najua namna ya kupromoti mwanamichezo afike juu kitu cha kwanza ni vyombo vya habari sasa mimi mwenyewe ni mwanahabari inawezekana;

Malinyi pia kunatakiwa kuwa na vikundi vya ngoma za kitamaduni za makabira yetu yaliyopo malinyi hii pia itasadia kutambulika utamaduni wa malinyi hata akija mgeni atajua tamaduni zilizopo malinyi

Kukuza pia vipaji vya sanaa kwa mfano Sanaa za Maonyesho, wasanii wa filamu na maigizo nao ni sehemu pia ya kukuza vipaji Malinyi, wapo pia waigizaji hawaonekani ni kwa sababu hawajapewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao tutakuwa na mpango maalumu Malinyi wa kubaini vipaji mbalimbali vya vijana wetu ili tuviendeleze.

Kwa kufanya hayo Malinyi itachanja mbuga kimaendeleo kadhalika tutawatazama pia wachongaji na wachoraji hizi zote ndugu zangu ni ajira ambazo zinaleta kipato kwa watu wetu wa Malinyi mpya na Mbunge Chaya inawezekana sana.

UWEZESHAJI WA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKUBWA

Kuwawezesha wajasiriamali ni kuwasadia katika mikopo midogo ili aweze kufanya biashara zao ili waweze kusonga mbele na kujiletea maendeleo yao wenyewe na jamiii yao

UMOJA ,UPENDO NA MSHIKAMANO

Tutaijenga Malinyi tukiwa wote tuna umoja upendo na mshikamano ndiyo itakuwa kazi yangu kwa watu wangu nitakaowangoza Malinyi kuwaleta pamoja,

Mwisho natawatakiwa wagombea wazangu kampeni za kistaarabu, tushindane kwa hoja tusitukanane tusiruhusu chuki, tusiruhusu wafuasi wetu wafanye fujo, sisi wagombea wote ni wa Malinyi, watoto wa baba mdogo na mkubwa kuna maisha baada ya uchaguzi, kusudi mshindi apatikane kwa haki na kwa matakwa ya wapiga kura wa Malinyi

Tumeanza na Mungu tumalize na Mungu, Mungu ibariki Tanzania Munga ibariki Malinyi asanteni kwa kunisikia".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news