Mgombea Urais Tanzania kupitia ADC, Queen Cuthbert Sendiga ataja maeneo watakayoanza kuyafanyia utekelezaji

QUEEN Cuthbert Sendiga ambaye ni mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atahakikisha wananchi wa Pemba watanufaika na zao la karafuu.

Amesema, Serikali yake itahakikisha zao hilo linapandishwa thamani ili liweze kuingiza fedha za kigeni na kuwafanya wananchi hao kuwa na maisha bora na kufurahia kuwepo kwa zao hilo.

Hayo ameyasema katika mkutano wa hadhara wilayani Micheweni kisiwani Pemba ambapo amesema kuwa, kwa kufanya hivyo itachangia kuwaingizia fedha za kigeni na kuwafanya wananchi hao kuwa na maisha bora.
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia ADC, Queen Cuthbert Sendiga.(DIRAMAKINI).

Pia amewaahidi wananchi kuwa atahakikisha wanapatiwa viwanda vya kusindika samaki ili kuweza kupata ajira za kutosha katika visiwa hivyo na kuwaondoa wananchi wa Pemba katika lindi la umasikini hasa wananchi wa Micheweni ambao kwa takwimu za kitaifa inaonesha wilaya hiyo ni maskini.

Sendiga amesema, Serikali atakayoiongoza kupitia ADC itafanya jitihada za makusudi kuhakikisha wananchi hao wanaondokana na umaskini ili nao waweze kuyafurahia maisha.

Pia katika kuhakikisha wananchi wanapata afya bora hasa kuepusha vifo vya mama na mtoto, amesema ADC itawekeza katika secta ya afya kwa upande wa Zanzibar ili kuhakikisha wananchi hao wanaondoka na kuzorota kwa afya zao.

Mgombea huyo pia amewataka Wanamicheweni na Watanzania wote kujihadhari na wanasiasa wanaoleta sera za uvunjifu wa amani.Queen amesema, wanasiasa hao waogopwe kama Corona na amesisitiza kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news