“Mimi ilani yangu inasema Mperampera spidi narudia chama chetu kinasema kipaumbele chake mperampera spidi, sisi UPDP, mkituchagua tu tukikaa ikulu kazi ya kwanza kabisa ndugu zangu nikupambana na wala rushwa kwa sababu rushwa ni adui wa haki;
Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP) Twalib Ibrahim Kadege ameahidi endapo atachaguliwa kuwa rais basi siku za mwanzo wataanza kupambana na rushwa.
Ameyasema hayo wakati akizindua rasmi kampeni za chama hicho jana Septemba 19, katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi na kusema kuwa ilani ya chama chao inaeleza jinsi ya kupambana na rushwa huku kauli mbiu ya chama hicho ikiwa ni mperampera spidi.
"Haya yote tunayo yalalamikia yanatokana na radhi ya rushwa, nchi yeyote duniani ikiwa na rushwa wananchi wake wanadhoofika, hawajiamini, hawajieliwi kwa sababu ya rushwa hii ndio kero kubwa sana,"amesema.