Waziri Mkuu mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi mjini Karatu katika mwendelezo wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.Mheshimiwa Pinda amewaambia wananchi wa Karatu wayapuuze madai
yanayotolewa na wapinzani kwa mgombea Ubunge wao, Daniel Awaki kuwa
hajui Kiingereza kwani Ubunge si Kiingereza na wala si lazima uwe na
Degree bali ujue kujenga hoja kwa maendeleo ya wananchi, anaripoti
Sophia Fundi (Diramakini) Karatu.
Amesema, Mgombea huyo ana uwezo
mzuri wa kujenga hoja na anaamini kupitia yeye chini ya uongozi wa Rais
Dkt.John Magufuli na madiwani wa CCM, Karatu inakwenda kung'ara kila
sekta baada ya Oktoba 28, mwaka huu.
"Hivyo niwaombeni ikifika
siku ya kupiga kura, kura zote mpeni Mgombea Urais, Mheshimiwa John
Magufuli, Mbunge Daniel Awaki na madiwani wote wa CCM, mtayafurahia
maendeleo na hakika msikubali kudanganywa kwa hoja ambazo hazina
mashiko,"amesema.