Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri, Jenerali Mahmoud Nassar,(mwenye suti) wakiwa na wataalamu mbalimbali kutoka nchini Tanzania na Misri wakiangalia picha mbalimbali za mradi mkubwa wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) Septemba 6,2020.
WAZIRI wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amesema ujenzi wa mradi
mkubwa wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) utakamilika kwa
wakati na kwa kiwango cha kimataifa, anaripoti HAFSA OMAR kutoka WN.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa kwenye mto Rufiji.
Katika ziara yake hiyo, aliambatana na Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri,Jenerali Mahmoud Nassar, Katiku Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Edward Ishengoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco, Dkt.Alexander Kyaruzi, Mkurugenzi Mtendaji Tanesco,Dkt Tito Mwinuka na wataalamu mbalimbali kutoka nchini Tanzania na Misri.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri, Jenerali Mahmoud Nassar,(mwenye suti) wakiwa na wataalamu mbalimbali kutoka nchini Tanzania na Misri wakiangalia picha mbalimbali za mradi mkubwa wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) Septemba 6,2020.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri, Jenerali Mahmoud Nassar,(mwenye suti) wakiwa na wataalamu mbalimbali kutoka nchini Tanzania na Misri wakiangalia picha mbalimbali za mradi mkubwa wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) Septemba 6,2020.
Aidha,alieleza kuwa tayari Serikali imemlipa mkandarasi wa mradi huo
zaidi ya trilioni 1.49, ambayo ni sawa na asilimia 100 ya malipo ambayo
mkandarasi huyo analitakiwa kulipwa kwasasa, ili kuhakikisha anafanya
kazi kwa kasi na kwa kiwango cha kimataifa.
“Tunataka mradi
ukamilike kwa wakati na kwa kiwango cha juu, sio mradi unakamilika baada
ya miezi miwili unanza kuhitaji tena ukarabati kwa gharama nyengine kwa
hili hatutakubali kwa hiyo nitoe wito kwa mkandarasi kufanya kazi kwa
weledi na kiwango cha juu,”amesema.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao baina ya ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Misri kabla ya kuanza kwa ukaguzi wa ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP),Septemba 6,2020. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco,Dkt.Alexander Kyaruzi.
Ujumbe kutoka katika Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani na ujumbe kutoka nchini Misri wakiongozwa na Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri, Jenerali Mahmoud Nassar wakikagua maeneo mbalimbali ya ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) Septemba 6,2020.
Ujumbe kutoka katika Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani na ujumbe kutoka nchini Misri wakiongozwa na Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri, Jenerali Mahmoud Nassar wakikagua maeneo mbalimbali ya ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) Septemba 6,2020.
Amesema kuwa, Serikali
imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo, ili
kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda ulipooangwa na kumtaka
mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi katika mradi huo.
Ujumbe kutoka katika Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani na ujumbe kutoka nchini Misri wakiongozwa na Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri, Jenerali Mahmoud Nassar wakikagua maeneo mbalimbali ya ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) Septemba 6,2020.
Naibu Waziri wa Ujenzi wa Misri, Jenerali Mahmoud Nassar akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza kukagua wa ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) Septemba 6, 2020. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani.
Katika
juhudi za kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati, Dkt. Kalemani
alitoa maagizo kwa mkandarasi pamoja na msimamizi wa mradi huo, maagizo
hayo ni pamoja na kuwataka waatalamu wote waliofanya kazi kwenye mradi
huo kufanya kazi kwa bidii na kumaliza kazi zao kwa wakati.
Pia,
amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha kuwa ifikapo mwisho wa
mwezi huu awe tayari amemaliza ujenzi wa handaki ujenzi huo ambao
ameuelezea kuwa muhimu ambao unategemewa kwa kiasi kikubwa kuendesha
mradi huo.
Vilevile, amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anajiri
waatalamu wote ambao wanahitajika katika ujenzi wa mradi huo na ifikapo
mwisho wa mwezi huo wawe tayari wamefika nchini kwaajili ya ujenzi huo.
“Hatuna
wasiwasi na ajira zinazotelewa hapa kwenye mradi hadi sasa umeajiri
watanzania zaidi ya 4500 kati ya watanzania 5500 na kwa wale waliobaki
waajiri ili kazi ziweze kwenda kwa haraka,”alisema Dkt.Kalemani.
Pia
ameagiza uharakishwaji wa ujenzi ya nyumba za wafanyakazi ambazo bado
ujenzi wake haujakamilika na kumtaka mkandarasi huyo kuzikamilisha kwa
haraka ili wafanyakazi wa mradi huo wahamie katika eneo hilo ambapo
itasaidia kufanya kazi zao kwa muda mrefu na mradi huo kukamilika
mapema.
Dkt.Kalemani amesema kuwa, mradi huo ndio utakaotatua
matatizo yote ya umeme nchini na kuahidi Serikali itasimamia kikamilifu
ujenzi wa mradi huo ambao utakuwa na faida kubwa na utapunguza
changamoto za umeme na utasaidia sana usambazaji wa umeme kwenye vijiji
na vitongoji nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi wa
Misri, Jenerali Mahmoud Nassar alisema, Rais wa nchi yao anafuatilia kwa
karibu utekelezaji wa mradi huo na yupo tayari kuhakikisha kuwa mradi
huo unakamilika kwa wakati.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said(kulia) Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Edward Ishengoma wakiwa katika kikao baina ya ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Misri kabla ya kuanza kwa ukaguzi wa ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP),Septemba 6,2020.
Aidha, amesema kuwa mradi huo
utakamilika kwa mafanikio makubwa kwa sababu ya ushirikiano mkubwa
wanaopata kutoka kwa Watanzania na kueleza kuwa mradi huo
utakapokamilika utaleta maendeleo makubwa nchini.
Pia amesema,
changamoto zote zilizojitokeza kwenye mradi huo watazifanyia kazi ili
kuhakikisha mradi huo unakamika wa kwa muda uliopangwa.
Naye
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said alisema maendeleo ya
mradi huo ni mazuri na changamoto zilizojitokeza zitafanyiwa kazi na
kuwataka Watanzania kuendelea kuunga mkono mradi huo wenye faida nyingi
katika katika Taifa letu.