NASA yajiandaa kumtuma mwanamke wa kwanza Mwezini kufanya uchunguzi

Zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 28 ( £22 bilioni) zinatarajiwa kuwezesha kufanikisha mpango wa wanaanga wa Marekani kufika mwezini. Mpango huo unatarajiwa kuwezesha wataalam wa kike na kiume kufika mwezini ikiwa ni awamu nyingine tangu mwaka 1972, anaripoti Mwandishi Diramakini.

(NASA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka Shirika la Anga za Mbali la Marekani (NASA) ambalo limebainisha litawatuma tena wanaanga wake mwezini.

Ingawa Mkuu wa NASA, Jim Bridenstine amesema hofu za kisiasa ni changamoto kubwa kwa kazi ya shirika lake. Rais wa zamani Barack Obama aliufuta mradi wa kupeleka wanaanga katika sayari ya Mars, baada ya mtangulizi wake kutumia mabilioni ya dola kuuandaa.

Kati ya fedha hizo, chombo cha kuwapeleka wanaanga hao kitagharimu dola bilioni 16. Mpango huo ulianzishwa na Rais Donald Trump kama mojawapo ya vipaumbele vya utawala wake huku hatua hiyo ikihitaji ruhusa ya Bunge la nchi hiyo ambayo inatarajiwa kufanya uchaguzi kabla ya mwezi huu.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa dola hizo zitapatikana kupitia bajeti ya miaka minne kati ya 2021 na 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news