NEC yafanya uamuzi wa rufaa 616 zilizowasilishwa na wagombea Ubunge na Udiwani

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha uchambuzi na kuamua rufaa za wagombea wa Ubunge na Udiwani. Hadi kufikia tarehe 17 Septemba 2020, baada ya kupitia kumbukumbu zote za rufaa zilizowasilishwa, tume inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania wote mambo yafuatayo,

"Jumla ya rufaa zilizopokelewa 616, ubunge zilikuwa rufaa 160,udiwani rufaa 456, malalamiko 23 na rufaa zilizojirudia 44.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Wilson Mahera Charles akisoma taarifa kwa umma kuhusu majumuisho ya rufaa za wagombea ubunge na udiwani Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Septemba 2020.

"Katika rufaa 160 za Ubunge zilizoamuliwa na tume matokeo yake ni kama ifuatavyo, wagombea waliorejeshwa ni 66, wagombea ambao hawakurejeshwa ni 32, rufaa zilizokataliwa za kuomba kuenguliwa wagombea ni 57 na rufaa zilizojirudia ni tano, hivyo jumla kuu ni 160;

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera Charles ameyasema hayo wakati akisoma taarifa kwa umma kuhusu majumuisho ya rufaa za wagombea ubunge na udiwani jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Septemba 2020.

"Kuhusu taarifa ya awali ya wagombea walioteuliwa kama wagombea pekee walikuwa 18. Baada ya tume kupitia rufaa zilizowasilishwa kutoka majimbo hayo, imerejesha wagombea watatu waliokuwa wameenguliwa katika majimbo ya Namtumbo, Bukene na Kavuu.

"Hivyo basi, majimbo hayo yataendelea na kampeni za uchaguzi utakaofanyika tarehe 28 oktoba 2020.

"Baada ta kupitia na kuamua rufaa mbalimbali, tume imekubali rufaa tatu za kuwaengua wagombea katika majimbo matatu.

"Kwa matokeo hayo wabunge waliopita bila kupigngwa ni 18. Pia tume imepokea taarifa ya kujitoa kwa wagombea wa Ubunge kwenye majimbo ya Chalinze na Madaba, hivyo kubakia wagombea pekee ambao wanakuwa wamepita bila kupingwa.

"Kufuatila kumalizika kwa kipindi cha pingamizi na rufaa, wagombea waliopita bila kupingwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ni 20. "Tume itawatangaza katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa sheria," ameyabainisha hayo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Wilson Mahera Charles.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news