Omary Mgumba:Ushindi wa mwaka huu CCM utakuwa wa kihistoria,makundi tupeni kule

NAIBU Waziri wa Kilimo,Omary Mgumba amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawana sababu ya kutokipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano,anaripoti HASSAN NINGA kutoka MOROGORO.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba akizungumza na wanachama./wwww.diramakini.co.tz

 

Mgumba amebainisha hayo wakati akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu Maalum ya  Wilaya ya Morogoro Vijijini,iliyokutana kwa ajili ya kuwaleta wanachama wa CCM pamoja ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi wa kishindo kuanzia udiwani,ubunge na urais.

 

Mgumba ambaye aligombea kuteuliwa kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki na kupata kura 242,Hamis Taletale (Babu Tale ) aliibuka mshindi na kuwa mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo na  kwa sasa ni mbunge mteule kutokana na kupita bila kupingwa katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki

 

Omary Mgumba amesema, sasa ni wakati wa kuondosha makundi ya kisiasa kwa kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi CCM kinapata ushindi wa kutosha.

Wajumbe wakionyesha ishara ya miaka mitano tena kwa CCM./wwww.diramakini.co.tz

Mgumba pia amesema Innocent Kalogelesi Mbunge mteule wa Morogoro Kusini  na Hamis Taletale wa Morogoro Kusini Mashariki wana nafasi kubwa ya kuhakisha hakuna makundi kwa kuwaweka watu kuwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa michakato ya kumpata atakayepeperusha bendera katika majimbo ya Morogoro Kusini,na Kusini Mashariki.

 

Katika hatua nyingine amesema kuwa, watahakikisha Mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt.John Magufuli anapata kura za kutosha kutoka majimbo hayo.

 

Amesema kuwa, wanaimaani kubwa kuwa majimbo hayo yataongoza kwa kumpigia kura Rais Magufuli kutokana na kile ambacho amekifanya ndani ya miaka mitano

 

Sanjari na hilo ameongeza kuwa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 imegusa sekta zote muhimu zenye lengo la kumkomboa mwananchi.

 

Nao baadhi ya waliokuwa watia nia katika majimbo hayo wameahidi kuungana na walioteuliwa na kuwa kitu kimoja ili kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapata kura za kutosha katika majimbo ya Morogoro Kusini na Kusini  Mashariki hasa katika urais na madiwani kwani tayari kuna wabunge wateule.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news