MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amesema iwapo Watanzania watakipa ridhaa chama hicho kupitia Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu miongoni mwa mambo ambayo Serikali ya Umoja wa Kitaifa itatekeleza kwa ufanisi ni pamoja na kufuta ushuru wote katika mazao ili kumuwezesha mkulima kupiga hatua.
Sambamba na kuhakikisha kilimo kinakuwa cha kisasa zaidi, hatua ambayo itawezesha uzalishaji kuwa mkubwa kwa manufaa ya wakulima na Taifa kwani malighafi nyingi za viwandani zinategemea kilimo.Lipumba ameyasema hayo leo Septemba 9,2020 wakati akiwahutubia wananchi mjini Kibaha mkoani Pwani ikiwa ni mwendelezo wa kuinadi sera ya chama hicho kuelekea Oktoba 28, mwaka huu.Zinazouwiana soma hapa.
Amesema, sera ya chama hicho ambayo imejikita katika haki sawa na furaha kwa wote, wamedhamiria kuwapa tabasamu wakulima, wavuvi na wafugaji ili kupitia shughuli zao waweze kufanikiwa haraka huku wataalam wa kilimo, mifugo na uvuvi wakipewa kipaumbele zaidi katika serikali hiyo.
Amesema, iwapo chama hicho kitapewa ridhaa wananchi ikiwemo wakulima mkoani Pwani wananeemeka kwa kuwa, licha ya kuwa na ardhi inayostawi mazao yote ikiwemo korosho bado tija yake ni ndogo.
PROFESA LIPUMBA:Mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu nitaanza kutekeleza haya mara moja
Tags
Siasa