WANANCHI visiwani Zanzibar wametakiwa kufahamu kuwa hakuna sehemu yoyote inayomkataza au kumzuia mwanamke kutokuwa kiongozi kwa misingi ya dini au kwa namna moja au nyingine.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA),Prof.Issa Haji Ziddy ameyasema hayo wakati alipokuwa akaizungumza na viongozi wa dini mbalimbali na baadhi ya wawakilishi kutoka asasi za kiraia katika ukumbi wa TAMWA uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Unguja jijini Zanzibar. Wanawake wanaweza kufanya maamuzi, soma hapa.
Walikuwa wanaangazia kuhusu uwasilishwaji wa muongozo wa utoaji wa elimu dhidi ya nafasi ya mwanamke na uongozi katika Uislamu nchini.
Amesema,kwa miaka mingi wanawake visiwani Zanzibar wamekuwa wakipoteza fursa za uongozi kutokana na baadhi ya watu kwenye jamii kuwa na dhana potofu ikiwemo kuamini kuwa mwanamke hapaswi kuwa kiongozi jambo ambalo halina ukweli.
Amesema, wapo baadhi ya watu kwa sababu wanazozijua wao wanatumia baadhi ya aya za Quraan Tukufu kuwakandamiza wanake na kupelekea wanawake hao kupoteza fursa ambazo anaamini zingeweza kuwakomboa wao na familia zao pamoja na Taifa
‘’Hata mkataba wa hudaibiya ushauri wa makubaliano yale kwa mara ya kwanza ulitoka kwa mwanamke kwenda kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na wengi wa wanaume wakiwemo maswahaba walidhani wanakandamizwa, lakini ulikuwa mwanzo wa kheri kwa dini ya kiislamu,"amesema.
Ameongeza kuwa, hadi sasa kuna kundi kubwa la wanajamii wanaendelea kuamini kuwa kazi za mwanamke ni kutunza familia na wengine hawaruhusiwi hata kuwa viongozi kwenye mikutano ya familia zao.
Mjumbe wa Kamati ya Amani Zanzibar,Sheikh Fadhil Soraga amesema si sahihi wanawake kunyimwa fursa hizo na kuwa wanaofanya hivyo wanapaswa kutambua kuwa wanabeba dhima na wanapaswa kuacha mara moja.
Naye Baba Stanley Nicholas kutoka Kanisa la Angilaka Mkunazini mjini Unguja amesema yanayoendelea kutokea yote ni kwa sababu ya watu kutokuwa na elimu na kukosa utayari wa kujifunza, hivyo kuna kila sababu ya kubadilika na kuwapa nafasi wanawake kwa kuwa uwezo wanao.