Rais Dkt.John Pombe Magufuli na Rais Evariste Ndayishimiye wazindua jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma

Muonekano wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma ambalo limezinduliwa leo Septemba 19, 2020 kwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye.
Rais Magufuli amesema kabla ya kuzinduliwa kwa jengo hilo wananchi wa Kigoma walikuwa wakifuata huduma ya Mahakama Kuu mkoani Tabora, hivyo kulisababisha hata haki zao kuchelewa kutolewa, anaamini uzinduzi huo utawezesha wananchi kupata haki zao kwa wakati ikiwemo kuwapunguzia gharama za kusafiri.
Amesema, kuzinduliwa kwa Mahakama hiyo ni sehemu ya mkakati wa kujengwa kwa Mahakama nyingine katika maeneo mbalimbali nchini.
 
Rais amesema, lengo ni kusogeza huduma za kimahakama karibu na wananchi huku akisisitiza kuwa katika kipindi cha miaka mitano Serikali imeendelea kuimarisha muhimili wa Mahakama kwa kuongeza idadi ya majaji hadi kufikia 50 na mahakimu 938 nchini.

Pia ameitaka Mahakama kuhakikisha wanatunza miundombinu ya jengo hilo ambalo limejengwa kisasa na itumike katika kutoa haki badala ya kuipindisha haki kwa sababu za rushwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye wakifungua kwa pamoja jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma leo Septemba 19, 2020. (Ikulu).
 
Naye Rais wa Burundi, Evarist Ndayishimiye amesema, amekubali kufungua jengo hilo kwani ni heshima kubwa kwake na kwa wananchi wa Burundi.

Prof.Hamis Jumaa ambaye ni Jaji Mkuu Tanzania amesema kuwa, kukamilika kwa Mahakama hiyo kutarahisisha upatikanaji wa huduma za kimahakama kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambapo awali walikuwa wanafuata huduma hiyo Mkoa wa Tabora.
 
Wakati huo huo amesema, uzinduzi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma mkoani Mara ambalo nalo lililishakamilika na kuzinduliwa rasmi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news