Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Ali Mohamed Shein leo Septemba 18, 2020 amemuapisha George Joseph Kazi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, inaripoti Diramakini. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akimuapisha, George Joseph Kazi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo Septemba 18,2020 kabla alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria.(Ikulu Zanzibar).
Hafla ya kuapishwa kiongozi huyo ilifanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid
Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar pamoja na Mawakili wakiwa katika hafla ya kuapishwa George Joseph Kazi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar leo Septemba 18, 2020 katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar kabla alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. (Ikulu).
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Makatibu Wakuu.
Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe.Zubeir Ali Maulid wakati wa hafla ya kuapishwa, George Joseph Kazi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar kabla alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. (Ikulu).
Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Khatib Hassan, Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Saleh Juma Kinana, Washauri wa Rais wa Zanzibar, Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mawakili, viongozi wengine wa Serikali pamoja na wanafamilia.