Rais wa Marekani, Donald Trump ndani ya wiki hii amesafiri katika mji wa Kenosha, Wisconsin kuangalia madhara yaliyosababishwa na maandamano, kukutana na wakazi walioathiriwa na vurugu na kutembelea Kituo cha Dharura ikiwemo kushiriki katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wa jamii
Akiwa ziarani mjini humo,Rais Trump licha ya kutoa ple amesema utawala wake utatoa dola milioni moja kwa wasimamizi wa sheria mjini Kenosha, dola milioni 4 kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara wadogo ambao waliathirika na vurugu hizo na dola milioni 42 kwa kusaidia kuimarisha huduma na ulinzi ndani ya mji huo.
Ziara hiyo ya Rais Trump mjini Kenosha mapema wiki hii inafuatia vurugu kubwa ambazo zilitokana na watu ambao walikuwa wanalaani kupigwa risasi kwa Mmarekani mweusi, Jacob Blake ambaye ni mkazi wa mji huo, tukio lilosababishwa na mmoja wa maafisa wa polisi wa Kizungu mjini Kenosha.Picha zote na IKULU/www.diramakini.co.tz
Tags
Picha