MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha leo Ijumaa Septemba 11,2020
imemuachia kwa dhamana mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia
ACT-Wazalendo, Saed Kubenea.
SAED AHMED KUBENEA |
Kubenea alikamatwa Septemba 07, 2020 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo kuingiza fedha za kigeni bila kutoa tamko na kuingia nchini kinyume cha Sheria ya Uhamiaji. Aidha, kesi inayomkabili itatajwa tena Septemba 21, 2020.
Kwa nini mahakamani
"Hivyo, leo tarehe 7/9/2020, mara baada ya kujiridhisha na uwepo wa
ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa tajwa, sambamba na misingi ya
kikatiba inayoniongoza kama ilivyoanishwa katika Ibara ya 59B(4)(a)hadi
(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,
nimeidhinisha mashtaka yafuatayo dhidi ya mtuhumiwa SAED AHMED
KUBENEA:-a.
"Kuingia nchini Tanzania kinyume na Sheria ya
Uhamiaji, Sura ya 54 Marejeo ya mwaka 2016; na b.Kuingiza nchini fedha
za Kigeni bila kutoa tamko kinyume na Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha
Mpakani za mwaka 2016,"ameeleza Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania,Biswalo
Eutropius Kachele Mganga. Endelea kusoma hapa.