JAMHURI ya Serbia imetangaza kuwa, inatarajia kufungua mapema iwezekanavyo Ubalozi wake mjini Jerusalem ikiwa ni hatua moja wapo ya kuimarisha mahusiano ya kidplomasia na Israel.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameyabainisha hayo kupitia taarifa iliyoonwa na www.diramakini.co.tz mapema leo Jumapili Septemba 6, 2020.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Picha na PMO/www.diramakini.co.tz |
"Ninapenda kuwajulisha kuwa, ninayo furaha ya kipekee kuhusiana na mafanikio mengine makubwa katika juhudi zangu za kisiasa kwa Taifa langu. Rais wa Serbia, Alexander Wucchic ametangaza kuwa,Serbia itafungua ubalozi wake mjini Jerusalem mapema kabla ya Julai 2021,na kwa sasa juhudi zinaendelea.
"Hii ni nchi ya kwanza ya Ulaya kufungua Ubalozi wake mjini Jerusalem. Ninamshukuru sana rafiki yangu Rais wa Serbia Wucchic kwa maamuzi ya kukubali Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kuamua kuhamishia ubalozi wake mjini humo.
"Tutaendelea na juhudi zetu kuhakikisha mataifa mengine ya Ulaya yanahamishia balozi zao mjini Jerusalem. Vivyo hivyo, Waziri Mkuu wa Kosovo (Avdullah Hoti ) katika kikao na Rais Trump (Donald Trump wa Marekani) amemuhakikishia kuwa, Kosovo itafungua ubalozi wake mjini Jerusalem. Kosovo itakuwa nchi ya kwanza yenye Waislam wengi kufungua ubalozi wake mjini Jerusalem.
"Nilishasema haya tangu awali na niendelee kusema kuwa, maridhiano ya amani na kukubalika kwa Israel kunaendelea kushika kasi, hivyo tutarajie matokeo zaidi,"amebainisha Waziri Mkuu Netanyahu kupitia taarifa iliyoonwa na www.diramakini.co.tz
Tags
Kimataifa