Serikali yatoa maelekezo kwa waajiri wasiozingatia sheria za kazi nchini

"Katika siku za hivi karibuni kumeibuka baadhi ya waajiri wasiozingatia Sheria za Kazi kwa makusudi kwa kisingizio kwamba hawawajibiki chini ya sheria hizo.

Waajiri hao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa Maafisa Kazi wanapotekeleza majukumu ya kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi katika maeneo ya kazi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Jenista J.Mhagama. 

Aidha, waajiri hao wamekuwa wakitoa taarifa potofu kwa umma, viongozi wa Serikali na wanajumuiya wao kwa lengo la kudhoofisha juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa Sheria za Kazi zinafuatwa na kuzingatiwa nchini.

Ninapenda kuwakumbusha na kuwasisitiza waajiri wote kwamba wanapaswa kuzingatia na kutekeleza matakwa ya Sheria za Kazi.

Ninatoa rai kwa waajiri wote nchini kutoa ushirikiano kwa Maafisa Kazi wanapotekeleza majukumu yao ya kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi.

Aidha, iwapo kuna changamoto yoyote katika utekelezaji wa sheria, ninawasihi kuwasiliana na ofisi yangu badala ya kutoa taarifa potofu kwa umma, viongozi wa Serikali na wanajumuiya wao.

Ninaomba kuwahakikishia waajiri wote kuwa, Serikali yetu inathamini sekta zote ikiwemo Sekta Binafsi na Sekta ya Umma pamoja na Uwekezaji unaofanywa nchini kwa ustawi wa Taifa letu,"amefafanua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Jenista J.Mhagama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news