SPIKA JOB NDUGAI AZINDUA JENGO LA TAKUKURU MANYONI

Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwa ajili ya kuzindua jengo la TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na viongozi wa wilaya, watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua jengo la taasisi hiyo katika Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza na watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali (hawapo kwenye pichani) kabla ya uzinduzi wa jengo la taasisi hiyo Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Sabina Seja akizungumza na viongozi wa wilaya, watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali (hawapo kwenye pichani) kabla ya uzinduzi wa jengo la taasisi hiyo Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.



Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa baada ya kuzindua jengo la taasisi hiyo Wilaya ya Manyoni mkoani Singida. Wa pili kushoto waliokaa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa (kushoto waliokaa) na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja (wapili kulia waliokaa).

Spika wa Bunge, Job Ndugai (watatu kulia) akikata utepe wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja (wapili kulia) na Mbunge wa Manyoni Magharibi,Yahaya Masare.  PICHA NA OFISI YA BUNGE.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news