TAKUKURU yamrejeshea Mwalimu mamilioni ya fedha yaliyochukuliwa na wakopeshaji umiza

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Karatu Mkoa wa Arusha imemrejeshea mwalimu mstaafu fedha zake shilingi milioni 21.1 za mkopo umiza zilizoporwa na kampuni ya ukopeshaji ya Rhobi Credit Company Limitd ya mjini Karatu, anaripoti Sophia Fundi (Diramakini).

Mkuu wa Wilaya Karatu mkoani Arusha, Abbas Kayanda akimkabidhi mwalimu mstaafu Pilonga Visent fedha zilizorejeshwa in Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), fedha hizo zilizoporwa na Kampuni ya Rhobi Credit Company Limited ya mjini Karatu ambazo ni sehemu ya mafao yake.Fedha hizo zilirejeshwa na taasisi hiyo leo. (Diramakini).

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Sabas Salehe kupitia taarifa aliyoitoa ameeleza kuwa,kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya mafao ya mwalimu huyo ya kustaafu ambazo zilizoporwa na kampuni hiyo tangu mwezi Februari mwaka 2019.

Ameeleza kuwa, awali kampuni hiyo ilimkopesha mwalimu huyo kiasi cha shilingi milioni tatu mwezi Juni, 2018 kwa makubaliano kwamba angerejesha fedha hizo kwa riba ya asilimia 30 ambayo ni sawa na shilingi 900,000.

Salehe ameeleza kuwa, baada ya mstaafu huyo kupokea fedha zake za mafao kampuni hiyo ikampatia sharti lingine la kukabidhi kadi yake ya benki na namba ya siri kwa kampuni sharti ambalo mstaafu alilitekeleza.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baada ya fedha za mafao kuingizwa kwenye akaunti, kampuni hiyo ilichukua kiasi cha shilingi milioni 25 kama fidia ya deni na riba ya mkopo wa sh.milioni 3 iliyomkopesha Mwalimu Pilonga.

Atuganile Stephen ni Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Karatu amesema kuwa, walipokea taarifa ya mstaafu Pilonga akiwa amekata tamaa ya kutopata fedha zake zilizoporwa na kampuni hiyo na kuanza kuzifanyia kazi ambapo walipata uthibitisho na kuitaka kampuni hiyo kurejesha fedha za Pilonga kiasi cha sh.milioni 21.1, kiasi ilichokuwa imekichukua kwa ziada kinyume na makubaliano baina yake na mwalimu.

Mwalimu mstaafu Pilonga (aliyeshika fedha) akizungumza baada ya kupokea fedha zake alizorejeshwa na TAKUKURU wilayani Karatu na pembeni mwake kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Abbas Kayanda na kushoto kwake ni Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Sabas Salehe na Atuganile Stephen ambaye ni Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Karatu. (Diramakini).

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Abbas Kayanda akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha mstaafu huyo amewataka wananchi kuwa makini na makampuni ya ukopeshaji ambayo yanatoa mikopo umiza na watoe taarifa kwa wale wote ambao wamekubwa na mikopo ya aina hiyo.

Baada ya kupokea fedha hizo, mstaafu Pilonga amesema, anaishukuru TAKUKURU kwa kazi nzui ambayo wanafanya kwani alikuwa amekataa tamaa juu ya fedha zake hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news