TANESCO yamaliza tatizo la umeme Geita, RC Gabriel aeleza faida za hatua hiyo

MKUU wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa kuanza kutumika rasmi kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Mpomvu Mjini Geita itamaliza tatizo la uhaba wa umeme katika Mkoa huo, anaripoti Robert Kalokola (Diramakini) Geita.Kituo hicho kilichojengwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kinapokea umeme wa msongo wa Kilovoti 220 kutoka Bulyanhulu na kuupoza hadi Kilovoti 33 kwa ajili ya kuupeleka kwa watumiaji.

Akizungumza baada ya kuwasha kituo hicho rasmi Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa kulikuwa na mahitaji makubwa ya umeme katika mkoa huo,lakini kwa kitendo cha Tanesco kuwasha kituo hicho itamaliza malalamiko yote ya uhaba wa umeme.

Kituo hicho kimejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 50 ambacho umeme utakaotoka kwenye kituo hicho utakuwa na uhakika na kumaliza tatizo la umeme katika Mkoa wa Geita.

Amesema kuwa,malalamiko ya wateja wa umeme hasa wawekezaji kwenye sekta ya madini,viwanda na watumiaji wa kawaida yamepata suluhisho.

Meneja wa Miradi ya TANESCO,Mhandisi Emmanuel Manirabona amesema kuwa,umeme unaopozwa katika kituo hicho utaanza kusambazwa leo baada ya kuwasha rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Ameongeza kuwa ,umeme huo unasambazwa katika Mkoa wa Geita ambao mahitaji yake ni Megawati 16 na umeme mwingine utauzwa katika Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu wa Geita (GGML) na Stamigold na kubaki na umeme wa ziada.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news