Mhandisi wa Umeme
kutoka TANESCO, Hassan Kipende wa Idara ya AMR mita akieleza jambo wakati wa ukaguzi wa miundombinu
ya shirika hilo mkoani Pwani. |
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea na kampeni ya kutoa elimu juu ya matumizi bora ya umeme pamoja na kukagua miundombinu ya umeme na mota zinazotumiwa kwenye kuendesha mashine kwa wamiliki wa viwanda, machimbo ya madini na mashine za kusaga Mkoa wa Pwani, anaripoti NEEMA MBUJA.
Miongoni mwa elimu iliyotolewa ni pamoja na, namna ya kutumia vifaa ambavyo vinatumia umeme kidogo, umuhimu wa kukagua mota zao mara kwa mara kwa ajili ya kuleta ufanisi na usalama wa miundombinu.
Kuhusu wachimbaji wadogo wa mawe eneo la Chalinze, Mhandisi Hassan Kipende aliendelea kuwapatia elimu ya umuhimu na faida ya kutumia umeme kwani wengi wao bado wanatumia mafuta kuendesha mitambo ya kuchakata mawe jambo ambalo ni hasara kwao.
Tags
Uchumi