LEO Septemba 16,2020 kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga nchini (TCAA), Hamza Johari, ameainisha kurejeshwa kwa huduma za usafiri wa ndege kwa nchi jirani.
Uamuzi huo unatokana na Waraka wa Serikali ya Kenya uliotolewa jana Septemba 15, 2029 ulioindoa Tanzania katika nchi zilizokuwa zinatakiwa raia wake kuwekwa karantini kwa siku 14 wakiwasili nchini humo.
Taarifa ya Johari imetangaza kuondoa zuio la kutua nchini Tanzania kwa ndege zote kutoka Kenya zikiwemo za Kenya Airways,Fly 540 Limited, Safari Aviation na AirKenya Express Limited.Mzozo huo ulianza miezi miwili iliyopita baada ya mamlaka ya Kenya kuchukua hatua hasi kwa kuitenga Tanzania ilipofungua anga yake kwa kuwataka raia wake au wasafiri wakiingia Kenya lazima wawekwe karantini ya siku 14 kwa gharama zao.Lengo ni kuchunguzwa maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19).hUamuzi huo ulikuwa unazuia safari za Shirika la Ndege la Tanzania ATCL kwenda Kenya. Taarifa ya leo inaruhusu ndege zote za Kenya kutua Tanzania kuanzia sasa.