KOCHA wa Timu ya mpira wa miguu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC F,C Habibu Kondo amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kumenyana na timu ya Mbeya City siku ya Jumatatu katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/ 2021 katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yao leo, Kocha Habibu amesema kuwa muendelezo wa mazoezi hayo yatoa nafasi ya kwakwe ya kurekebisha mapungufu yanayojitokeza ili kukiweka sawa kikosi hicho kabla ya kukutana na wapinzani wao Septemba 7, mwaka huu.
Kocha huyo Mtanzania ameeleza kuwa timu hiyo kwa sasa haina mpinzani kutokana na uwezo, bidii walionao wachezaji hao na kwamba wana amini katika msimu huu timu hiyo itapata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kuchukua ubingwa. Zinazofanana soma hapa.
Ameongeza kuwa, katika msimu huu wa Ligi Kuu, timu hiyo ya KMC FC imefanyiwa maboresho makubwa ikiwemo kurekebisha kasoro ambazo zilijitokeza katika msimu uliopita na kwamba mashabiki wategemee kupata burudani.
Tags
Michezo