KAMPUNI ya Mafuta ya Total Tanzania imezindua kituo kipya cha huduma ya mafuta, Total Mchigani eneo la Goba jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika leo Septemba Mosi,2020.
Total Tanzania imekuwa ikihimiza wamiliki wa biashara kukuza biashara zao kwa kuingia ubia wa kibiashara na kampuni hiyo kwa njia ya DODO ambayo itawawezesha kumiliki na kuendesha vituo vya mafuta vyenye chapa ya Total.
Mfumo huu unawawezesha wafanyabiahsara kuingia kwenye ubia na kampuni ya Total na kuweza kumiliki, kuendesha pamoja na kusimamia vituo vya huduma vya mafuta vyenye chapa ya Total.
Kituo hicho kipo kwenye moja ya barabara yenye shughuli nyingi za kiuchumi jijini Dar es salaam inayotokea Mbezi Beach hadi Mbezi Kimara hivyo kulenga kuwahudumia wakazi wa Tegeta, Mbezi Beach na Kimara pamoja na watumiaji wote wa barabara hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Jean Franchois Schoepp amesema, Total inalenga kumfikia kila Mtanzania na kuwapatia nafasi ya kufuruhia huduma na bidhaa nzuri kutoka Total.
"Leo, tunafurahia kuingia katika ubia wa kibiashara na Mhandisi Frank Malle ambae ni mmiliki wa kampuni ya F.S Mshuwa Co na mmiliki wa kituo hichi. Kwa ushirikiano huu tunatarajia kuihudumia Goba na jamii inayoishi maeneo ya jirani.
Kuhusu Total Tanzania
Total Tanzania ni kampuni ya mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya shirika hilo.
Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total katika kujitanua kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya Total Tanzania Limited kupitia mradi wake wa Total Access to Solar (TATS) project, inasambaza taa za nishati jua zinazoitwa AWANGO kwa jamii ya Watanzania
Pia kampuni ya Total imenunua kampuni ya GAPCO Tanzania pamoja na kiwanda cha kutengeneza vilainishi nchini ili kuzidi kuwafikiwa Watanzania kwa urahisi na kuwapa huduma na bidhaa zenye ubora.
Kuhusu Kampuni ya Total
TOTAL ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ni ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote.
Ina wafanyakazi 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni, kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.
Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.
Total imeanzisha kampeni kabambe utafutaji na uzalishaji wa mafuta kwa kuongeza idadi ya visima vya mafuta huku ikijitahidi kupata nishati endelevu kwa ajili ya Bara la Afrika kwa sasa na baadae.
Total imejikita katika uhamasishaji wa utafutaji vya vyanzo vipya vya nishati kutoa kipaumbele cha elimu ya nishati kwa vijana ili kuendeleza uwezo wa kipekee wa bara hili la Afika kujiletea maendeleo.
Mbali na hilo,Kampuni ya Total ndio wasambazaji wa kwanza wa bidhaa za mafuta (mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa , lami, na GPL, nk) katika bara la Afrika.
Shukrani kwa mizizi yake ya kihistoria, ubora wa bidhaa na huduma zake, kutoka jumla ya vituo 4200 vya mafuta katika nchi 40 barani Afrika.
Vituo vya mafuta vya Total ni vituo tegemeo kwa wafanyabiashara binafsi na wateja wake. Lengo letu ni kuwezesha upatikanaji mkubwa zaidi wa nishati, ambayo pia inahusisha kuendeleza upatikana wa vyanzo vingi na mbadala vya nishati na kwa gharama nafuu kama vile nishati ya jua, kwa kuuza vifaa vya nishati ya jua.
Total tunasikiliza mahitaji ya wadau wetu, na sisi kwenda nao pamoja nao katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi, ajira, elimu na afya. Zaidi www.total.com