Tundu Lissu ambaye ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amewaeleza watumishi, wakulima, wafanyabiashara na wavuvi kuwa, iwapo watampa ridhaa Oktoba 28, mwaka huu atahakikisha ndani ya siku chache baada ya kuanza majukumu yake Ikulu wanapata haki zote.
"Mkinichagua nitahakikisha ninawapa haki yenu ya nyongeza ya mishahara sanjari na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na hawajapandishwa, vivyo hivyo nitahakikisha wafanyabiashara wengi ambao wamefilisika kwa sababu ya kutozwa kodi kubwa ninawaondolea machungu hayo;
Amesema,watumishi wa Serikali na wananchi wote atahakikisha wanatendewa haki ili kila mmoja aweze kujiletea maendeleo yake.
Lissu amesema, njia nyingine atakayotumia ni kuhakikisha anaziondoa sheria zote ambazo zinaonekana kuwa kandamizi kwa wakulima na wavuvi, hivyo kuwakosesha haki zao kila wanapotaka kupiga hatua.
"Hivyo ndugu zangu, kura zote ifikapo Oktoba 28, mwaka huu nipeni mimi kwa nafasi ya urais, Ubunge hapa Chief Kalumna na madiwani wote wa CHADEMA, pia kule vijijini mpeni kura zote Conchesta Rwamlaza na madiwani wake ili tukawatumike,"amesema.