MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema akishinda katika Uchanguzi Mkuu mwaka huu atahakikisha maslahi ya wakulima,wafugaji, wavuvi,wajasiriamali wadogo, watumishi wa umma wakiwemo wataalam wa afya nchini wanafurahia kazi za mikono yao.
"Na hili ndilo agano
langu kwa watu wa Mwanza na Kanda ya Ziwa, wavuvi Serikali yangu
haitataifisha nyavu zenu bali italinda haki zenu, na nyie machinga
mnaofanya biashara kwenye mitaro nitawatengenezea mazingira mazuri hivyo
mchague CHADEMA pia walimu,manesi na madaktari maslahi yenu
nitayatetea ilani yetu ya uchaguzi inasema Uhuru na Haki, kwani bila
huru wananchi wa Tanzania hawawezi kusema wapo huru bila ya kupata mambo
nilioyataja,"ameeleza Lissu.
Lissu ameyasema hayo leo jijini Mwanza katika mwendelezo wa kampeni za chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.
Amesema,endapo watashinda serikali yake itahakikisha wakulima wananufaika na zao la pamba na kupata bei halali na soko la uhakika pamoja na kupata vifaa kuchambulia zao hilo ili ziweze kuwa na ubora wa hali ya juu.
Pia amesema, Serikali yake itapiga marufuku machinga kuuziwa vitambulisho na kuwatoa kwenye mitaro kwa kuwajengea majengo makubwa ya kibiashara na kila machinga atagawiwa eneo lake popote nchini.
Tags
Siasa