Umoja wa Falme za Kiarabu kufungua Ubalozi nchini Israel

MMOJA wa maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) amesema muda wowote kuanzia sasa wanatarajia kufungua ubalozi nchini Israel. Ikiwa ni hatua ya kuimarisha ushirikiano zaidi baada ya makubaliano ya hivi karibuni ya kihistoria.Rejea hapa kwa ufahamu zaidi.

Kwa mujibu wa Gazeti la Hayom la Israel limemnukuu afisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe wa Wizara ya Mambo ye Nchi za Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu akisema hayo na kuongeza kuwa, baada ya kufunguliwa ubalozi huo, Waisrael wataanza kuitembelea nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi bila kikwazo.

Mshauri wa Masuala ya Usalama Israel, Meir Ben-Shabbat (kushoto) wakiagana na mmoja wa maafisa wa Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Abu Dhabi juzi.Picha na wmfe.

Pia amekaririwa akisema kuwa,umoja huo unatafakari juu ya suala la kufungua pia ubalozi mdogo ama katika mji wa Haifa au Nazareth ili kurahisisha shughuli hizo za kibalozi baina ya pande hizo mbili.

Hivi karibuni Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilieleza kuwa, maafisa wake, Marekani na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa pamoja wameridhia hatua hizo za ufunguzi wa balozi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news