Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), upepo wa Pwani
unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka
Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Mashariki kwa Pwani
ya Kusini, vivyo hivyo hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi
makubwa kiasi.Pia hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua vinatarajiwa
katika maeneo mengi.. TMA inabainisha kuwa, matarajio kwa siku ya Jumapili
ya
Septemba 20, 2020 kutakuwa na mabadiliko kidogo. |