Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), upepo wa Pwani
unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kutoka
Kusini Mashariki kwa Pwani yote, vivyo hivyo hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo.Ngurumo zinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa ziwa Victoria. TMA inabainisha kuwa, matarajio kwa siku ya Jumatatu
ya
Septemba 21, 2020 kutakuwa na mabadiliko kidogo.