Vijana 1,539 wahitimu mafunzo ya kijeshi wilayani Arumeru, DC Muro awataka kuyatumia mafunzo hayo kwa maslahi ya Taifa



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro akitoa hotuba ya kufunga mafunzo ya kijeshi ya Wahitimu 1539 katika Kikosi cha 833 KJ Oljoro Septemba 18,2020. Hao ni wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, Operesheni Uchumi wa Kati wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amewataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyoyapata katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii ikiwemo kudumisha amani na usalama kwenye maeneo yao na ujenzi wa Taifa kwa ujumla.

Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi -CDF, Brigedia Jenerali Ibrahim Mabele akisoma salaam maalum za Mkuu wa Majeshi.

Kaimu Kamanda wa Kikosi Luteni Kanali J.P. Meidimi akisoma taarifa ya mafunzo ya wahitimu.

Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya amewataka wahitimu hao, kutumia haki yao ya kikatiba kwenda kushiriki na kupiga kura katika Uchaguzi huu ifikapo Oktoba 28, 2020, huku akihimiza kuwachagua viongozi ambao wamefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwa taifa letu ikiwemo kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati, kama iliyokuwa jina la operesheni yao (Operesheni Uchumi wa Kati - 2020). Mafunzo hayo, yalihusisha uhodari, uzalendo, umoja na uzalishaji mali.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akisalimiana makamanda wa Kikosi cha Oljoro alipowasili kikosini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akikaribishwa rasmi kukagua gwaride la Wahitimu.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akikagua gwaride la wahitimu hao Septemba 18, 2020.


Wahitimu walipata fursa ya kuonesha jinsi walivyoiva katika mbinu zote za medani ikiwemo kupita vizuizi hatari na mapigano bila ya matumizi ya silaha.



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro alipata fursa ya kuwazawadia wahitimu bora wawili katika ukakamavu na pia mafunzo ya kijeshi kwa ujumla.



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro alipata pia fursa ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ufugaji wa kuku wa kikosi hicho.


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro katika jukwaa kuu pamoja na makamanda wakiangalia maonesho ya ukakamavu yaliokuwa yakioneshwa na wahitimu.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Jerry Muro akibadilishana mawazo na baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo ambayo yalianza Agosti 17, 2020 na kufungwa Septemba 18, 2020 na mkuu huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news