Pamoja na mambo mengine
kikao kilijadili na kupitisha matumizi ya Mfumo wa Malipo Serikalini
(MUSE),tathmini ya utendaji kazi kwa wafanyakazi kwa mwaka 2019/20 na
rasimu ya taratibu za uendeshaji wa misiba.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya (katikati) akiendesha kikao cha 14 cha Baraza la Wafanyakazi, Septemba 17, 2020 katika Ukumbi wa Baraza uliopo chuoni hapo. Kushoto ni Katibu wa Baraza, Bi.Stellah Masanja na kulia ni Katibu Msaidizi, Wakili Gulliver Simime.Wakati akifunga kikao, Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni
Mkuu wa chuo, Prof. Hozen Mayaya aliwashukuru na kuwapongeza wafanyakazi
wote wa chuo kwa utendaji kazi wao mzuri katika kipindi kilichopita na
kuwaasa waendelee na moyo huo huo wa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na
weledi wa hali ya juu ili kuona malengo ya chuo na Taifa ya kuzalisha
wataalamu bora wa masuala ya mipango ya maendeleo wanaokidhi mahitaji
ya soko.
Pichani Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakifuatilia kwa makini
majadiliano wakati wa kikao hicho Septemba 17, 2020.Picha ya pamoja Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof.Mayaya (katikati walio kaa) na Wajumbe wa Baraza. Kulia kwa Mwenyekiti ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) Taifa, Dkt. Paul Loisulie na kushoto kwa Mwenyekiti ni Katibu Msaidizi wa RAAWU-Kanda ya Kati, Bi.Diana Kweka.
Wafanyakazi Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wapewa mbinu za kufikia matokeo chanya nchini
Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Septemba
17, 2020 limefanya kikao chake Cha 14 katika Ukumbi wa Baraza Jengo la
Pili la Taaluma, Kampasi Kuu Dodoma.
Tags
Picha