Wananchi Karatu wataja sababu za kuwanyima kura wapinzani kuanzia udiwani hadi Urais

WANANCHI katika Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo wamemuomba Mgombea Ubunge kupitia CCM atakaposhinda aitafutie ufumbuzi kero ya maji,anaripoti PIUS NTIGA (KARATU).

Jimbo la Karatu kwa muda wa miaka zaidi ya ishirini na tano limekuwa chini ya upinzani, hivyo wamesema hali hiyo imechelewesha huduma za kijamii ikiwemo maji.




Huduma ya maji inayopatikana sasa ni ya visima vya kuchimbwa ambavyo havitoshelezi wananchi wa Karatu.

Wakizungumza na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM Mjini Karatu wananchi hao wamesema Oktoba 28, mwaka huu hawatafanya makosa kwani Chama Cha Mapinduzi kimempitisha Mgombea anayekubalika na wananchi wa Karatu ambao wengi ni wakulima wa vitunguu,hivyo wanaimani na CCM.

Wananchi hao wameomba pia barabara kwani zilizopo hasa za vijijini hazipitiki vizuri sambamba na kuwekewa lami katika baadhi ya barabara zilizopo Mjini Karatu ili kupunguza vumbi lililopo Mjini humo.

Kutokana na hali hiyo,Mgombea Ubunge Jimbo la Karatu Kupitia CCM, DANIEL AWAKY, ambaye pia ni MNEC,  amesema atakaposhinda  uchaguzi Mkuu wa mwaka huu changamoto ya barabara, umeme pamoja na maji atazitafutia ufumbuzi wa kina na kuhakikisha Karatu inakuwa na maendeleo ya haraka kwa kuwa ni mji ambao ni kitivo cha utalii nchini.

Aidha, Mgombea huyo wa Ubunge kupitia CCM amesema kabla ya kugombea Ubunge amekuwa akisaidia wananchi hususani wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo, hivyo amewaomba Kura ili afanye maajabu makubwa kwa wanakaratu.

Amesema serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli itaibadilisha Karatu.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Karabu, Shaban  Mrisho, amejivunia mtaji wa wanaccm zaidi ya Elfu 60 waliojiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura kuwa wataipigia Kura CCM na hivyo kuwa na Imani ya kulikomboa Jimbo la Karatu.

"Zaidi ya wananchi Milioni moja na Elfu Arobaini wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura la time ya Taifa ya Uchaguzi" alisema katibu wa CCM.

 "Michezo michafu na usaliti ndani ya CCM ulifanya Jimbo la Karatu kwenda upinzani hivyo kasoro hizo ndani ya Chama zimefanyiwa kazi chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli, hivyo mwaka huu ushindi Ni wa asubuhi tu,"amesema.

Aidha, Mrisho amesema umoja na mshikamao uliopo katika Jimbo la Karatu unakipa ushindi CCM kwani safari hii kimempitisha mgombea ambaye ni mkulima anayekubalika kwa wapiga kura wa karatu ambaye ni Daniel Awaky.

Kuhusu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 imetekelezwa vizuri kupitia sekta ya utalii ambapo zaidi ya Hotel sitini kubwa za kitalii zinauweka mji huo kuwa kitovu Cha utalii na hicho kuchangia mapato ya mji wa karatu.

Amesema Wilaya ya Karatu hapakuwepo na Hospitali ya Wilaya, ambapo sasa inajengwa na ipokatika hatua za Mwisho kukamilika.

"Zamani huduma za Afya walikuwa wakizipata kupitia vituo vya Afya au kwenda Wilaya jirani ya Mbulu Mkoani Manyara kwa ajili ya kupata matibabu, sasa hali hiyo haitakiwepo tena" alisema

"Kura yako ndio maendeleo yako, wajitokeze kwa wingi watu wenye sifa ya kupiga kura wakapoge Kura Oktoba 28 mwaka huu,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news