Zaidi ya wanawake 1,700 mkoani Iringa wamejipanga kuhakikisha
wanazitafuta kura za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Dkt.John Pombe Magufuli ili aweze kuwa Rais wa Tanzania, anaripoti Fredy
Mgunda (Diramakini),Iringa.
Akizungumza kwenye kongamano hilo
mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Telesia
Mtewele amesema wanawake wa Mkoa wa Iringa wanapaswa kuyaeleza mambo
ambayo Rais Magufuli amefanya kwa kipindi cha miaka mitano.
Amesema
kuwa, Rais Dkt.Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa
elimu bure,kukarabati majengo ya shule na kujenga majengo mapya mengi na
amefuta michango shuleni hivyo wanawake wa Iringa wanapaswa kumtafutia
kura Dkt.John Pombe Magufuli.
Mtewele ameongezea kwa kusema kuwa
katika sekta ya elimu wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wanapata mikopo
kwa wakati na ndio maana kwa kipindi cha miaka mitano hakuna maandamano
ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ilivyokuwa miaka ya huko nyuma.
Amesema
kuwa, Rais Dkt.John Pombe Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya afya
kuwa kujenga vituo vya afya zaidi ya 400,hospitali za wilaya,kuongeza
bajeti ya dawa kwenye hospitali zote,kuajiri wafanyakazi wa sekta ya
afya na ameboresha huduma za upasuaji kwenye hospitali zote za rufaa
hivyo wanawake wanajifungua bila shida kama ilikuwa hapo awali.
Mtelewe
amewaomba wanawake wa Mkoa wa Iringa kutumia ushawishi wao kuhakikisha
wanampigia kura nyingi mgombea huyo wa chama cha mapinduzi, Dkt.John
Pombe Magufuli kwa kuwa ana uwezo wa kuliongoza taifa hili kimaendeleo
kuliko wagombea wengine.
Mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Telesia Mtewele akiongea na wanawake waliojitokeza kwenye kongamano hilo la kimkakati la kutafuta kura za wagombea wa CCM. (Diramakini).
Amewaomba wanawake wa Mkoa wa Iringa kwenda kuzitafuta kura za CCM
kuanzia udiwani,ubunge hadi urais hivyo wanawake waliohudhuria kongamano
hilo lilikuwa na lengo la kuhakikisha CCM inapata kura za kutosha
kuliko vyama vingine.
"Kauli mbiu yetu ni wanawake wa Iringa
tunakwenda na Magufuli na ndio lengo la kongamano hilo ni kuhakikisha
tunatafuta kura za kutosha kuliko vyama vingine vyote na kuendelea
kushika dola kama ilivyokuwa kawaida ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM),"amesema.
Baadhi ya wanawake waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano hilo la kimkakati la kutafuta kura za wagombea wa CCM. (Diramakini).
Naye Mratibu wa Kongamano hilo, Ritta Kabati amesema kuwa mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika nchi hivyo wanawake wa mkoa wa Iringa wameamua kumuunga mkono mgombea huyo.
Amesema kuwa, zaidi ya wanawake 1,700 walijitokeza kwenye kongamano hilo ambao lilifikia lengo la kuhakikisha wanawake wa mkoa wa Iringa wanazitafuta kura za chama cha mapinduzi kwa njia yoyote ile ili kuwapa ushindi wagombea wa CCM.
"Kongamano hilo liliwakutanisha wanawake kutoka kwenye sekta mbalimbali kama vile wafanyabisha,wanawake wanaouza kwenye baa,grocery,vilabuni,dini,taasisi, walemavu, machinga, wakulima, walimu,madaktari na wengine, hivyo kongamano hilo lilifanikiwa kugusa sekta zote,"amesema Kabati.
Kabati amewaomba wanawake wa mkoa wa Iringa waendeleee kuwaelimisha wananchi wengi ambao wanapiga maendeleo yalifanywa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ili waweze kumpigia kura nyingi mgombea huyo ashinde kwa kishindo.
Aidha, Kabati amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano aliyokuwa Rais amefanikiwa kuboresha sekta zote kwa kiasi kikubwa hivyo wanawake wa mkoa wa Iringa wanapaswa kuzitafuta kura nyingi za mgombea huyo wa CCM.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu amesema mwanamke ni nguzo kubwa katika amani ya jamii kwa kuwa mara zote amekuwa akijishusha katika mambo mbalimbali na hivyo kuleta amani.
Msambatavangu amesema wanawake wa Iringa wana kila sababu ya kuwachagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kimewahudumia vizuri na pia kimeonesha kutaka kuwahudumia vizuri kutokana na ilani ya chama hicho ya mwaka 2020 hadi 2025.